LIVERPOOL, ENGLAND
LOUIS VAN GAAL (pichani chini) ameponda
utaratibu uliotumika kumuondoa katika nafasi yake ya ukocha klabuni Manchester
United na kisha Jose Mourinho kurithi mikoba yake.
Mholanzi huyo
alitimuliwa baada ya kuwa na misimu miwili migumu Old Trafford kuponda ujio wa Mourinho
klabuni hapo kufanywa siri na maofisa wa klabu hadi uteuzi wake ulipothibitishwa
rasmi.
Van Gaal anaamini
suala hilo lingeweza kuchukuwa kwa njia tofauti na lilivyofanywa ingawaje anaamini
mrithi wake hana hatia na kuondolewa kwake ghafla.
Bosi
huyo wa zamani wa Old Trafford alikuwapo uwanjani Anfield Jumamosi katika mchezo wa upinzani wa jadi
kati ya Liverpool na United ulioisha kwa sare ya 0-0 akiwa ni sehemu ya timu ya
Runinga ya Uholanzi iliyokuwa ikirusha mchezo huo.
Van Gaal na Mourinho walikutana
uwanjani hapo kabla ya kuanza kwa mchezo huo, lakini kocha huyo bado hajasau jinsi
alivyoondolewa klabuni hapo na nafasi yake kuchukuliwa na msaidizi wake huyo wa
zamani klabuni Barcelona.
Van Gaal alisema: “Kwa
hisia zangu, jinsi usajili wake kama kocha wa Manchester United haukuwa sahihi
kabisa, hilo ndilo lililosababisha mimi kufukuzwa.
“Katika kanuni, yeye (Mourinho)
siyo mtu mbaya. Anaweza kuwa na huruma na alikuwa hivyo wakati alipokuwa
msaidizi wangu siku za nyuma. Lakini sasa anajisahau haraka mno.”
Mholanzi huyo
alifukuzwa baada ya ushindi wa Kombe la FA na pamoja na utawala wake kukabiliwa
na upinzani, bado ana kumbukumbu nzuri.
Van Gaal aliongeza: “Nilikuwa
na wakati mzuri na uhusiano wangu na wafanyakazi wote na mashabiki ulikuwa
mzuri wakati nilipokuwa United.”
“Mkurugenzi wetu mtendaji,
Ed Woodward aliniahidi chupa sita za mvinyo mwekundu wa Ribeiro kila nilipoifunga Liverpool. Vizuri, nilishinda mara nne, kwa hiyo nilikuwa na chupa
nyingi."
Post a Comment