0
Gazeti la Marca likionyesha thamani ya jezi ya Madrid.
MADRID, HISPANIA

REAL Madrid inajipanga kukubali dili jipya la vifaa vya michezo vya adidas ambalo itaifanya miamba hiyo ya La Liga kuvuna Pauni 106 milioni kwa mwaka, kwa mujibu wa ripoti kutoka Hispania.

Ronaldo
Dili hilo litakuwa kubwa zaidi na la aina yake, likiifunika  makubaliano  ambayo adidas alisaini na Manchester United majira ya joto mwaka 2014.
Klabu hiyo ya Old Trafford, ilianza kuvaa jezi na kutumia vifaa vya adidas msimu huu baada ya miaka 13 ya ushirikiano na Kampuni ya Nike, ilikubali dili la miaka 10  na adidas ya Ujerumani huku kila mwaka ukiwa na thamani ya  Pauni 750 milioni.
Rooney akiwa na jezi ya adidas

Lakini kama kiasi kilichochapishwa na Gazeti la Marca Ijumaa kama kiko sawa, dili la Real Madrid litaiondoa United na kuwa klabu yenye makubaliano bora ya vifaa vya michezo.
Inadhaniwa Real na adidas wako mbioni kuingia makubaliano ya miaka10, likihusisha Pauni1kwa alama. 
Ukurasa wa mbele ya Gazeti la Marca limechapishwa picha ya jezi ya Real Madrid ikifuatiwa na kichwa cha habari: ‘Jezi yenye thamani kubwa zaidi duniani.'
Dili hilo litaifanya Real Madrid ilirejee kwenye nafasi yake ya juu ya kuwa na jezi yenye thamani kubwa katika makubaliano  baada ya kuipoteza kwa Manchester United mwaka 2014.
Kwa mtazamo huu, jezi ya Real Madrid itakuwa na thamani zaidi kwa klabu za Chelsea, Arsenal na Liverpool hata kama zitachanganywa pamoja.
Real Madrid ilisaini mkataba mpya na adidas mwaka 2012 ambao ulikuwa uendelee hadi mwaka 2020 lakini mkataba mpya utachukua nafasi hiyo mwishoni mwa msimu huu. 

Miamba ya Bundesliga, Bayern Munich ilisaini mkataba wa miaka 15 na adidas msimu uliopita wa majira ya joto ambao una thamani ya Pauni 60 milioni kwa msimu.
Mkataba wa makubaliano kati ya adidas na Mtendaji Mkuu wa Man, United, Ed Woodward yalifanyika wakati timu hiyo iposhindwa kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini kampuni hiyo imekadiria kuuza jezi zenye thamani ya Pauni 1.5 billioni baada ya mkataba huo, ambao utaanza mwaka ujao.
Wazalishaji vifaa wa Man United waliopita Kampuni ya Nike ofa yao haikuweza kufua dafu kwa adidas na kuendelea kushirikiana na Man United kutokana na mkataba wao uliokuwa na thamani ya Pauni 30 milioni kwa miaka 13.
Manchester United inapambana msimu huu kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa ingawaje imeshuka hadi nafasi ya tano ikidaiwa ni kutokana na mfumo wa ufundishaji chini ya kocha Louis van Gaal na kusababisha kukosolewa  mwezi uliopita na Mtendaji Mkuu wa adidas, Herbert Hainer.
''Biashara na Man United inakwenda vizuri sanal,” aliliambia Gazeti la Suddeutsche Zeitung. “Tunauza jezi zaidi ya tulivyotegemea, mauzo ya nje ni wastani wa asilimia 60.
“Tunaridhika, ingawaje uchezaji wa Man United sio ule hasa tuliotazamia kuuona.”



 

Post a Comment

 
Top