0


BARCELONA, HISPANIA
UNAKUMBUKA jinsi Cristiano Ronaldo alivyokuwa akienda Morocco kwa kutumia ndege yake binafsi kumtembelea rafiki yake bondia, Badri Hari?
Kitendo hicho kilihusishwa na ushoga baada ya Ronaldo kupiga picha zilizozua utata na rafiki yake huyo.
Basi katika mchezo wa El Classico wa Jumamosi iliyopita staa huyo wa Real Madrid alizomewa uwanjani Camp Nou na kelele hizo kulaumiwa na bodi ya kupinga ubaguzi ya Hispania.
Bodi hiyo (StopLGBTfobia) imeitaka serikali ya Hispania kuchukua hatua dhidi ya watu waliokuwa wakipiga kelele za kupinga ushoga zilizosikika wakati wa dakika za kuomboleza msiba wa mkongwe wa Barcelona, Johan Cruyff.

Ronaldo 
Makelele hayo hayakuandikwa kwenye ripoti ya mwamuzi wa mchezo huo ambao Madrid ilishinda mabao 2-1 na si Ronaldo wala klabu yake waliozungumzia  kitendo hicho.  
Hata hivyo, Mkurugenzi wa  StopLGBTfobia, Francisco Ramirez amesema hatua zinapaswa kuchukuliwa  kukabiliana na vitendo vibaya vya unyanyasaji ambavyo vinasambaa katika viwanja vya Hispania.
"Vitendo hivi vya aibu na kutisha vinaweza kutolewa adhabu chini ya sheria ya michezo ya mwaka 2007," Ramirez alisema.
"Hiki si kitu kipya katika viwanja vya Hispania, ambapo kwa miaka kadhaa wachezaji na waamuzi wamekuwa wakitukanwa na kubaguliwa, pasipo na kutolewa adhabu yoyote ya mfano. Hii (adhabu) itamaliza kuendelea kwa ubaguzi katika soka la Hispania."

Mashabiki wa Barca wakimzomea Ronaldo, pamojana kuwafunga.
 Ramirez alidai Ronaldo alikuwa mlengwa wa kelele hizo za  kupingwa kwa ushoga kutoka kwa mashabiki wa timu pinzani na waandishi wa habari waliokuwa wakijaribu kumtukana na kumkebehi nahodha huyo wa Ureno.
"Kwa miezi kadhaa, Ronaldo ameendelea kutukanwa na kutajwa katika tetesi za magazeti na vyombo vya habari vinavyopenda skendo, lakini pia kwa waandishi wa michezo, wachezaji na mashabiki wa timu pinzani,  kwa lengo la kumdhalilisha, kumfedhehesha na kumdhalilisha mchezaji huyo mkubwa," alisema.
"Ni dhahiri kwamba matumizi ya kutumia mambo ya kijinsia ni kama siraha yenye lengo la  kumtukanisha na kumdhalilisha.
“Siku za nyuma jambo kama hilo lilitokea kwa wachezaji waliosumbuliwa na kutukanwa kama hivyo, mfano mchezaji na kocha wa zamani wa Barcelona (Pep) Guardiola  na viungo wa zamani wa Madrid, Guti na Michel.

Kumbe hata Guardiola?
"Siyo wakati huo wala sasa kumechukuliwa hatua yoyote ya kuondoa doa hilo katika michezo. Ni muhimu kufafanua kwamba ubaguzi watu wanaobaguliwa nao ni mashoga tu. Badala yake watu wanaamini, au kutumia kutukana ili kuwasumbua wanyonge."
Tume ya Kupinga Ubaguzi katika Michezo Hispania ilianzishwa mwaka 2007 kukabiliana na matatizo ya ubaguzi, ubaguzi wa rangi na chuki, na siku za hivi karibuni ilianza kutoa adhabu kwa watu wanaopiga kelele za kibaguzi na au kuonesha ishara hizo katika michezo.
Wasimamizi wa Ligi ya La Liga wamewahi kuwalalamikia mashabiki wa Real Madrid walioimba ‘Messi siyo mtu kamili’ katika Uwanja wa Santiago Bernabeu mwezi Novemba katika mchezo wa El Clasico.

Guti naye...
Na pia mashabiki wa Barcelona waliowahi kuimba ‘Cristiano mlevi’ wakati wa mchezo dhidi ya Levante katika Uwanja wa Camp Nou, Februari 2015.
StopLGBTfobia imesema mamlaka bado haijachukulia kama unyanyasaji dhidi ya ushoga ni tatizo halisi katika soka.
Katika mchezo huo, Ronaldo alifunga bao la ushindi baada ya Karim Benzema kusawazisha bao la Gerard Pique.

Post a Comment

 
Top