Atletico imepoteza mchezo wa kwanza wa robo fainali uliochezwa Jumanne baada ya kufungwa mabao 2-1.
Suarez, akiwarudisha katikati ya uwanja.
Straika wa Atletico Madrid, Fernando
Torres alifunga bao katika dakika ya 35 na kutolewa nje dakika saba baadaye kwa
kadi nyekundu wakati timu yake ikiongoza bao 1-0.Luis Suarez alifunga mabao yote mawili ya Barcelona, lakini kabla ya hapo alionekana akimgombana na beki wa Altetico Madrid, Juanfran.
Torreeeees
"Sijui wachezaji wa Barcelona
wanatakiwa wafanye nini ili waweze kutolewa nje kama sisi," alisema beki
wa kushoto wa kimataifa wa Brazil, Luis.Bingwa mtetezi, Barcelona, imepanga kuwa timu ya kwanza kushinda taji la Ligi ya Mabingwa mara mbili mfululizo, ikihitaji ushindi mwembamba katika mchezo wa marudiano uwanjani Vicente Calderon Jumatano ijayo.
....akishangilia bao
Atletico ilifunga bao la kuongoza
kupitia kwa Torres, lakini mchezo ulibadilika baada ya straika huyo wa Hispania
kuoneshwa kadi za mbili za njano za kipuuzi ndani ya dakika saba.Kocha wa Atletico, Diego Simeone alipandwa na hasira dhidi ya mwamuzi wa mchezo huo Mjerumani, Felix Brych, ambaye alishindwa hata kumkemea Suarez aliyekuwa akimsumbua beki wa kulia wa Atletico, Juanfran.
...akioneshwa kadi nyekundu,(hayupo pichani).
"Hatukupaswa kupewa kadi
nyekundu, kwa jumla haikuwa sawa," alisema beki za zamani wa Chelsea,
Luis."Siyo kitu chepesi kucheza dhidi ya Barcelona katika Ligi ya Mabingwa. Tunajua ni hatari kama watatoka robo fainali. Tunapaswa kucheza dhidi ya kila mmoja na kila kitu.
"Unaweza kuwaambia kuwa kuna hofu kwamba Barca inaweza kuondolewa."
...akitoke nje
Luis alikubali kwamba Atletico inakabiliwa
na kazi ngumu kutinga nusu fainali lakini aliongeza: "Bado tuko vizuri. Inawezekana."Simeone alisema hakuchukizwa na Torres, pamoja na kwamba straika huyo mwenye umri wa miaka 32 aliyewahi kuzichezea Chelsea na Liverpool baadaye aliomba msamaha.
Post a Comment