MANCHESTER,
ENGLAND
KOCHA
wa Manchester United, Jose Mourinho ameripotiwa kujiandaa kumvua kitambaa cha
unahodha straika wake Wayne Rooney hata kama ataendelea kubaki kwenye timu hiyo
kwa msimu ujao.
Hatima
ya staa Rooney mwenye umri wa miaka 31 ipo mashakani huko Man United baada ya
msimu uliopita kushindwa kujitengeneza namba ya kudumu na msimu ujao kuna
uwezekano mkubwa akawekwa mbalimbali zaidi kama ataamua kubaki na timu hiyo.
Kwa
kipindi cha karibuni, Rooney amekuwa akihusishwa na mpango wa kuhamia kwenye
Ligi Kuu China au kwenda katika klabu yake ya zamani ya Everton baada ya
kuonekana hatakuwa na nafasi kwenye kikosi cha Mourinho kwa msimu ujao.
Kutokana
na hilo, Mourinho anaripotiwa kwamba tayari ameshachagua wachezaji watatu ambao
mmoja wao atarithi kitambaa hicho cha unahodha wa Man United.
Majina
hayo matatu yanayoaminika kuchaguliwa na Mourinho ni Michael Carrick, Ander
Herrera na Paul Pogba.
Rooney
amekuwa kwenye kikosi cha Man United tangu alipojiunga na timu hiyo akiwa
kijana mdogo mwaka 2004 na alikuwa nahodha wa timu hiyo ilipokuwa chini ya
kocha Louis van Gaal mwaka 2014 baada ya kuondoka kwa Rio Ferdinand na Nemanja
Vidic na Ryan Giggs kustaafu.
Rooney
Post a Comment