LIVERPOOL, ENGLAND
PHILIPPE COUTINHO (pichani chini)
ameachwa katika kikosi cha Liverpool kilichosafiri Jumatatu kwenda Ujerumani
katika mchezo wa hatua ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Hoffenheim,
na kuongeza wasiwasi wake wa kubaki Anfield.
Coutinho mwenye umri
wa miaka 25- alikosa mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu England ambapo Liverpool
ilitoka sare ya mabao 3-3 na Watford Jumamosi kutokana na kuwa na majeraha.
Hata hivyo,
kukosekana kwake kunazua wasiwasi na kuhusishwa na jaribio lake la kutaka kujiunga
na Barcelona.
Liverpool imesema
Coutinho hauzwi. Wamiliki wa klabu hiyo Fenway Sports Group wametoa taarifa
kuthibitisha kuwa staa huyo wa kimataifa wa Brazil ataendelea kuwa mchezaji wa
timu yao hadi mwisho wa dirisha la usajili baada ya kukataa ofa ya Euro100
milioni (Pauni 90.4 milioni) kutoka Barcelona.
Hata hivyo, taarifa
hiyo imetolewa kufuatia ujembe wa barua pepe kutoka kambi ya Coutinho, kiungo
huyo wa zamani wa Inter Milan anataka kwenda Nou Camp katika usajili huu wa
majira haya ya joto.
Habari hizo zitakuwa
ni sawa na wimbo katika masikio ya maofisa wa Barcelona, wanaojipa matumaini kuwa
kitendo cha mchezaji huyo kuomba kuondoka kitabadilisha mawazo ya Liverpool katika
mkakati wake wa kugomea ili aruhusiwe kutua Hispania.
Hata hivyo, Coutinho hatazuiwa
kuitumikia Barcelona katika Ligi ya Mabingwa Ulaya hata kama ataichezea
Liverpool katika mchezo wa marudiano wiki ijayo.
Shirikisho la Soka la
Ulaya limewaruhusu wachezaji kuwakilisha klabu zao katika hatua ya makundi na
ile ya kufuzu.
Mchezaji
mwingine aliyeachwa na Kocha Jurgen Klopp ni Daniel Sturridge, ambaye anauguza
majeraha baada ya kuumia katika maandalizi ya msimu dhidi ya Bayern Munich.
Post a Comment