0


              LIVERPOOL, ENGLAND
PHILIPPE COUTINHO hatimaye anakamilisha taratibu za kutua Barcelona kwa uhamisho wa Pauni 145 milioni kutoka Liverpool.
Picha za kiungo huyo mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil zimemuonyesha akisafiri Jumamosi jioni akitokea London kwenda Hispania kukamilisha taratibu za mwisho za dili hilo.
Kutokana na pande zote mbili kukubaliana, Coutinho amejifunga Barcelona kwa miaka mitano na nusu na atakuwa na kifungu kinachomruhusu kuondoka kwa Euro 400 milioni (sawa na Pauni 355 milioni).
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amefunguka jinsi kiungo huyo alivyokuwa akilazimisha kuondoka tangu dirisha lililopita
 “Coutinho alikuwa akinisistizia mimi, wamiliki wa klabu na hata wachezaji wenzake kuhusu kuruhusiwa akajiunge na Barcelona. Sisi kama timu tulikuwa tunasita kujiandiaa kuachana na rafiki yetu mzuri, mtu mzuri na mchezaji mzuri, Philippe Coutinho.
“Siyo siri Philippe alitaka kuondoka tangu Julai, wakati Barcelona ilipomtaka kwa mara ya kwanza,” alisema Klopp.
“Pamoja na hivyo, tuliweza kumbakisha mchezaji huyo hadi dirisha la majira ya joto, tukiwa na matumaini tungeweza kumsahawishi kuendelea kubaki na kuwa sehemu ya kile tunachotarajia kukifanya.
“Naweza kuwaambia mashabiki wa Liverpool sisi, kama klabu tumefanya kila tunachoweza kumshawishi Philippe kubaki na kuwa sehemu ya Liverpool na kutokwenda Hipsania.
“Lakini kwa asilimia100, bila shaka maisha yake ya baadaye– na yale ya familia yake– yanahusiana na Barcelona. Ni ndoto yake na sasa nimeamini hakuna chochote kilichasailia kinachoweza kumshawishi kubali mtazamo wake.”
Barcelona imethibitisha dili hilo kwa kuonyesha video akionyesha jezi ya Coutinho imetundikwa karibu na ile ya wachezaji wenzake katika chumba cha kubadilishia nguo, baadaye ikaachia video nyingine katika Mitandao ya Twitter na Instagram.

                                        ...akitua Barcelona
Ni usajili wa pili ghali duniani kwa muda wote, nyuma ya Mbrazili mwenzake Neymar aliyeihama Barcelona kujiunga na Paris Saint Germain (PSG)kwa ada ya uhamisho ya Pauni 198 milioni katika dirilisha la majira ya joto lililopita.  

... akiondoka London
Pia, ni usajili wa ada kubwa kwa wachezaji wasiokuwa na kifungu cha ada ya uhamisho katika mikataba yao na ameiingizia Liverpool faida ya kuvutia, ambayo ilimsajili kutoka Inter Milan kwa Pauni 8.5 milioni mwaka 2013. 
Uhamisho huo pia umevunja rekodi kwa klabu za Kiingereza, kwa Barcelona kulipa karibia Pauni 106 milioni kwanza na nyongeza baadaye.

akiwa na wakala wake, Kia Joorabchian 
Barcelona ilijipanga kulipa Pauni 97.5 milioni na nyongeza ya Pauni 35 milioni lakini Liverpool ilifanikiwa kuongeza dau kwa Wakatalunya hao baada ya tovuti ya Kampuni ya Nike ambao ndio wadhamini wa Barcelona kufanya makosa na kumtangaza Mbrazili huyo ni mchezaji wa Barca kabla ya makubaliano.

...akiwa na mkewe Aine London
Katika pesa za ziada Liverpool itavuna Pauni 17.7 milioni kama Coutinho atacheza michezo 100, ukiongeza na kiasi cha Pauni 4.4 milioni kwa kila mechi mbili za kwanza za Ligi ya Mabingwa Ulaya Barca itakazofuzu na kwa kila mechi mbili za itakazoshinda Kombe la Uerope League.

Kwa mara ya kwanza Coutinho anaweza kuonekana uwanjani Alhamisi katika mchezo wa Kombe la Hispania dhidi ya Celta Vigo.
Hata hivyo, hataweza kuitumikia Barcelona katika Ligi ya Mabingwa ingawaje kushiriki kwake kwenye michuano ya Copa del Rey na Ligi ya La Liga kutakuwa muhimu kuelekea Kombe la Dunia mwaka huu.

Kusajiliwa kwake kutamfanya Andres Iniesta – mchezaji ambaye atakwenda kurithi siku za baadaye – kupumzika kwa ajili ya michuano ya kimataifa. Pia, ataungana na Luis Suarez ambaye alikuwa rafiki yake ya wa karibu walipokuwa Merseyside.  
Katika dirisha la majira ya joto, msimu uliopita Klopp alisema Coutinho hataruhusiwa kuondoka na alikataa ofa kadhaa kutoka Barcelona ambazo zilifikia hadi Pauni 114 milioni­­.
Wamiliki wa Liverpool, Fenway Sports Group walifanya tukio lisilo la kaiwada kwa kutoa taarifa kuwa mchezaji huyo asingeweza kuuzwa katika dirisha hilo la usajili. 
Coutinho anaondoka Anfield akiwa amefunga mabao 54 katika michezo 200 ndani ya jezi ya Liverpool, pamoja na kwamba hajashinda taji lolote.

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post a Comment

 
Top