0

MADRID, HISPANIA
REAL Madrid imejaribu mara tatu have katika miaka mitano kumsajili  supastaa wa Barcelona Lionel Messi, kwa mujibu wa ripoti kutoka Hispania.
Wawakilishi wa Madrid walijaribu kumsajili Muargentina huyo mwaka  mwaka 2011, 2013 na  2015, lakini Messi aliwakatalia katika kila jaribio.
Messi, ambaye ameshinda tuzo ya tano ya Ballon d’Or akiwa mchezaji bora wa dunia, amekuwa mchezaji muhimu kwa mafanikio ya Barcelona kwa miaka ya hivi karibuni,  baada ya klabu hiyo  kutwaa Kombe la Mabingwa wa Ulaya, Kombe la Ligi na Copa del Rey.

Ripoti hiyo imesema jaribio la kwanza la Madrid lilikuwa mwaka 2011 wakati  straika wao, Cristiano Ronaldo alipokuwa akihusishwa kujiunga na Manchester City.
Pia, Juni mwaka 2013 ilidaiwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Real Madrid  alipewa maelezo na Rais  Florentino Perez – kufanya jaribio lingine kumsajili baada ya kushindwa na Barcelona katika mbio za kumnasa Neymar na with Ronaldo kuonyesha kutokuwa tayari kwa ajili ya mkaba mpya.
Jaribio la mwisho lilifanyika mwaka jana, kwa mujibu wa ripoti hiyo, baada ya Barcelona kutawala Ulaya na Real kushindwa vibaya nyumbani.
Kitendo cha Messi kuwagomea Real Madrid mara kwa  mara kimeelezwa kuwa ndiyo sababu ya miamba hiyo ya Hispania kujaribu kumgeukia Neymar kwa siku za karibuni. Real Madrid imetenga Pauni 144.4 kwa ajili ya Neymar.

 

Post a Comment

 
Top