0


                         MANCHESTER, ENGLAND
JOSE MOURINHO (pichani chini) kwa mara ya kwanza amefunguka kuwa hatamalizia kazi yake ya ukocha akiwa Manchester United.
Bosi huyo wa Old Trafford alidokeza kuna maisha ya kufanya kazi sehemu nyingine baada ya kumaliza kibarua chake Old Trafford.
“Kitu pekee ninachoweza kusema ni kuwa, bado miye ni kocha mwenye matamanio na nia ya kufanya vitu vipya na kupata changamoto mpya,” Mourinho aliiambia TV ya Ufaransa, Channel TF1.
“Nina uhakika sitamalizia kazi yangu hapa (Manchester United).”
Mourinho ambaye tayari ameshafanya kazi kubwa na kuandika historia katika nchi za Ureno, Italalia, Hispania na England, alifanya mahojiano hayo kwa Lugha ya Kifaransa na kuenezwa katika Jiji la Paris, pia aliulizwa kuhusu uwezekano wa kujiunga na PSG.
 “Mtoto wangu wa kiume anayeishi London aliamua kwenda Paris na sio Manchester kutazama mechi hivi karibuni. Kwanini Paris?

“Kwa sababu PSG ina kitu maalumu. Ina ubora, ina vijana, kila vitu vizuri,” aliongeza kocha huyo.
Mreno huyo alijiunga na United katika majira ya joto 2016 kufuatia kutimuliwa kwa mtangulizi wake, Louis van Gaal, alisema ana hamu ya kujaribu vitu vipya na kitu hicho kinaweza kuwa ni kwenda Paris.
Mourinho alisaini mkataba wa miaka mitatu na aliirudisha United katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. Katika Ligi Kuu England nited iko nyuma ya Manchester City kwa pointi mbili baada ya michezo minane.

Kwa sasa PSG inanolewa na Kocha, Unai Emery, aliyeingia makubaliano ya mkataba wa miaka miwili na uwezekano wa kuongeza miezi 12- Juni 2016 aliporithi mikoba ya Laurent Blanc. 

Post a Comment

 
Top