Neymar akiitumikia Barcelona
BARCELONA,
HIPSANIA
STRAIKA
wa Barcelona, Neymar amesema anamzimikia kocha Pep Guardiola na anapenda
kucheza chini yake.Neymar na Guardiola hawajawahi kukutana Nou Camp, wakati Mbrazili huyo alipotua akitoka Santos mwaka 2013, mwaka mmoja nyuma Guardiola alishaondoka.
Baada ya mwaka mmoja Neymar akiwa na Barcelona, Guardiola akachukua majukumu ya kuifundisha Bayern Munich lakini sasa imebainika kuwa ataondoka katika klabu hiyo ya Ujerumani mwishoni mwa msimu na kwenda kufundisha soka England.
Guardiola mwenye umri wa miaka 44 amekuwa
akihusishwa na Chelsea baada ya kufukuzwa kwa Jose Mourinho na pia ametakiwa na
Manchester City na Manchester United.
"Guardiola
ndiye mtu ambaye kwa kweli ninayemzimikia na ningependa kufanya naye kazi,"
alisema Neymar.Na aliongeza: "Ni vigumu kusema kwamba nataka kucheza katika nchi nyingine. Hakuna mtu anayeijua kesho, lakini nina furaha sana hapa nilipo sasa, Barcelona.
"Ninataka kurudi Brazil siku moja na pia ninataka kucheza Marekani, katika nchi hizo mbili ndipo ninapotamani kucheza baadaye."
Neymar amekuwa vizuri kwenye kikosi cha
Barcelona msimu huu baada ya kufunga mabao16 katika La Liga katika mechi 20
ilizoichezea timu yake.
Post a Comment