LISBON, URENO
CRISTIANO RONALDO yuko kwenye dunia nyingine kabisa ya
soka kwa sasa. Jumatano aliiongoza Ureno kushinda mabao mawili na kuipeleka timu
yake ya taifa Ureno kwenye fainali za Kombe la Dunia litakalofanyika Russia.
Lakini, wakati Ronaldo akifanya yake uwanjani dhidi ya Uswisi
jijini Lisbon, jukwaani kulikuwa na mgeni mashuhuri ambaye alikuwa akishangilia
mabao hayo na kuibua gumzo.
Ni mwanamuzi nyota duniani raia wa Marekani, Lady Madonna, ambaye
alifunga safari na kuungana na mashabiki wa Ureno kuipa sapoti hiyo ambayo kwa
sasa imekuwa kwenye kiwango cha juu kabisa.
Madonna alikuwa sambamba na mwanaye wa kiume David Banda, ambaye
yuko kwenye kikosi cha timu ya vijana ya Benfica, akiendelea kujifua huku
akionyesha kiwango cha juu.
nyota huyo wa kike mwenye kila aina ya vituko, alimuasili Banda
kutoka Malawi mwaka 2006, pia ana mtoto wa kike aliyemuasili kutoka Ureno.
Banda aliyekuwa amevaa jezi namba 7 inayovaliwa na Ronaldo,
alipelekwa Kituo cha Benfica baada ya kuonyesha kiwango bora katika soka tangu
akiwa kinda.
Ureno imekaa patamu katika Kundi B. Beki wa Arsenal Johan
Djourou, alijifunga dakika ya 41 kisha Andre Silva akapiga bao la pili dakika
ya 57.
Post a Comment