MANCHESTER,
ENGLAND
PAUL
POGBA (pichani chini) amesisitiza kuanzia sasa atakuwa mchezaji muhimu Manchester United baada
ya kutua mzigo wa mchezaji ghali zaidi duniani mabegani mwake.
Pogba alikuwa
mchezaji ghari zaidi duniani aliporudi United akitokea Juventus katika dirisha
la usajili majira ya joto msimu uliopita kwa dau lililovunja rekodi la Pauni 90
milioni.
Dau hilo kubwa
lilikuwa mzigo katika kupambana kutimiza majukumu yake- pamoja na kwamba United
ilishinda mataji matatu msimu ulioisha.
Lakini usajili wa
kushtua wa Neymar wa Pauni 200 milioni kutoka Barcelona to Paris St Germain (PSG)
unamaanisha utamrudisha Pogba mchezoni kuliko kwenye suala la dau alilonunuliwa.
Pogba alisema: “Msimu
ulioisha swali la kwanza kutoka kwa kila mtu lilikuwa ni kuhusu bei niliyonunuliwa.
“Sasa kila mmoja
atazungumzia kuhusu soka. Hii imaanisha kila kitu.”
Na Pogba amesema mambo mazuri yanakuja
kutoka kwake na sasa ana majukumu ya kuisaidia United kushinda taji la Ligi Kuu
kwa mara ya kwanza tangu 2013.Kiungo huyo aliyeondoka Juventus mwaka 2012, alisema: “Nimekuja hapa kushinda kushinda Ligi Kuu na kujipa changamoto mwenyewe.
“Nataka kufanya vizuri uwanjani, lakini ni kwa jinsi timu inavyotaka.”
United ni moja ya timu inayopewa nafasi ya kushinda taji la Ligi Kuu msimu huu na Pogba alisema vijana hao wa Jose Mourinho wana nia ya kufanya hivyo.
Hata hivyo, Pogba amewataka wasibweteke baada ya ushindi wao wa kushindo wa mabao 4-0 dhidi ya West Ham katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu wikiendi iliyopita.
Post a Comment