LONDON,
ENGLAND
CHELSEA
imekaa chini na kutafakari kisha kuamua kumrudisha kikosini straika wake, Diego
Costa.
Inadaiwa
bosi mkuu wa mabingwa hao wa Ligi Kuu
England, amemwamuru Costa kurejea London na kujiunga na kikosi hicho na kufanya
mazoezi na kikosi cha kwanza baada ya kugoma akiamini hicho kitakuwa kipimo
kama anataka kuuzwa Altetico Madrid.
Chelsea
imetoa masharti manne kwa Costa ambaye amegoma kurejea London na kubaki Brazil.
Taarifa
iliyotolewa Jumanne na uongozi wa klabu hiyo imeeleza Chelsea imempa masharti
manne staa huyo mwenye asili ya Brazil.
Diego
Costa anatakiwa kurudi London kujiunga na wenzake mazoezini, aimarishe kiwango
chake kwenye mechi na aongeze juhudi ili kuwapo kikosi cha kwanza.
Jumatatu
Diego Costa aliuambia Mtandao wa Daily Mail kuwa amehudhunishwa jinsi
anavyochukuliwa kama mhalifu na timu hiyo baada ya kufukuzwa kwa SMS na Kocha
Conte.
Costa
alisema, Chelsea ilimwekea masharti ya kufanya mazoezi na wachezaji wa akiba,
kutoruhusiwa kuingia katika vyumba vya kubadilishia nguo vya wachezaji wa kikosi
cha kwanza na kutozungumza nao.
“"Wanataka nikafanye mazoezi na kikosi cha akiba, siruhusiwi kabisa
kuwasogelea mastaa wa kikosi cha kwanza. Mimi siyo mhalifu, sidhani kama ni
haki kunifanyia hivi kwa mambo yote niliyowafanyia," alikaririwa Costa.
Chelsea
imeshampiga faini Costa ya Pauni 300,000 kwa kushindwa kuripoti klabuni wiki
mbili zilizopita kwa kukata mshahara wake anaochukua Pauni 15,000 kwa wiki.
Straika
huyo alisema hajali na anachotaka ni kuondoka bure kujiunga na timu yake ya
zamani ya Atletico Madrid.
Hata hivyo,
agizo hili la kiongozi wa juu wa Chelsea huenda likamrudisha Costa mazoezini
muda wowote tangu lilipotolewa Jumanne.
Costa aliwahi
kutuma video katika mtandao wake wa Instragam akionekana akifanya mazoezi
katika ufukwe wa Brazil.
Katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu, Chelsea ilichezea kichapo cha mabao 3-2 kitu ambacho kinaweza kuwa sababu ya straika huyo kurudishwa kundini.
Post a Comment