MADRID, HISPANIA
SHIRIKISHO la Soka la
Hispania limepigilia msumari wa mwisho katika uamuzi wake wa kumfungia straika
wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo michezo mitano.
Ronaldo alifungiwa
mechi moja baada ya kutolewa katika mchezo wa kwanza wa Super Cup wa Hispania
Jumapili lakini aliongezewa mingine minne- kwa kufanya kosa la kumsuma mwamuzi
wa mchezo huo, Ricardo de Burgos kwa nyuma baada ya kuonyeshwa kadi
nyekundu.
Supastaa huyo wa Real
Madrid atakosa mchezo wa marudiano wa Super Cup dhidi ya Barcelona Jumatano
usiku, na pia atakosa michezo minne ya kwanza ya La Liga, ambapo Real Madrid itaanza
na Deportivo La Coruna Jumapili.
Madrid ilikata rufaa
kupinga kadi ya pili ya njano aliyopewa Ronaldo katika mchezo wa ushindi wa
mabao 3-1 dhidi ya Barcelona uwanjani Camp Nou.
Ronaldo alipewa kadi
hiyo baada ya kujiangusha wakati akipambana na beki Samuel Umtiti ili kupata penalti
lakini hakufanikiwa.
Kabla ya tukio hilo,
Ronaldo alipewa kadi ya kwanza ya njano baada ya kuvua jezi alipokuwa akishangilia
bao la pili alilolifunga katika mchezo huo.
Ronaldo baada yakufunga bao la pili.
Kocha
wa Madrid, Zinedine Zidane alihoji
kitendo cha Shirikisho la Soka la Hispania kumfungia Ronaldo michezo mitano.
“Tunachopaswa kufanya
ni kusubiri kesho,” Zidane alisema. “Kamati inakutana asubuhi. Baada ya hapo
tutajua cha kufanya. Nimekatishwa tamaa. Sote tumekatishwa tamaa. Siku zote
sipendi kujihusishwa na waamuzi lakini unapoona mambo kama haya yanavyotokea...
Zidane amehoji Ronaldo kufungiwa mechi tano.
“Tutaenda kuzungumza
na kamati kuhusu jambo hili vizuri. Unapofikiria kuwa hatacheza michezo mitano
kwa ajili yetu, kuna kitu kinaendelea.
“Imenisumbua na
imetusumbua sote. Ni michezo mingi sana kwake na hilo ndilo ninalolisema.”
Post a Comment