RIO DE JANEIRO, BRAZIL
DIEGO COSTA (pichani chini) amesema hawezi kurudi klabuni
Chelsea wakati hatima ya maisha yake bado haijawekwa sana klabuni hapo.
Fowadi huyo mwenye miaka 28 kwa sasa amerudi kwao
alikozaliwa huko Brazil na amegoma kurudi England kuungana na timu yake baada
ya kocha Antonio Conte kuamua kumwengua katika kikosi chake cha kwanza.
Costa hakuwapo hata kwenye tukio la upigaji wa
picha wa kikosi hicho cha kwanza cha Chelsea kwa msimu huu.
Straika huyo aliyeamua kuichezea Hispania katika
soka la kimataifa, alipaswa kurudi klabuni Chelsea wiki mbili zilizopita ili
kwenda kufanya mazoezi katika kikosi cha akiba kufuatia kuzuiwa kabisa
kuwasogelea wachezaji wa kikosi cha kwanza.
"Wanataka nikafanye mazoezi na kikosi cha akiba,
siruhusiwi kabisa kuwasogelea mastaa wa kikosi cha kwanza. Mimi siyo mhalifu,
sidhani kama ni haki kunifanyia hivi kwa mambo yote niliyowafanyia,"
alisema Costa.
"Wamenipa wiki moja zaidi, lakini baada ya hapo
wataniadhibu. Wanataka nikafanye mazoezi kwenye kikosi cha akiba, siwezi kwenda
kufanya hivyo. Sina makosa, hivyo kama wanataka kuniadhibu kwa kunipiga faini,
basi waache tu wafanye hivyo.
"Nitakubali adhabu hiyo ya kila wiki, lakini
siwezi kuendeshwa kwa pesa. Kitu muhimu kwangu ni furaha jinsi ninavyoishi,
nipo hapa na wazazi wangu na hao ndiyo watu wanaoniheshimu. Nitakaa Brazil hata
mwaka mzima bila ya kucheza na kama Chelsea watanitoza faini kwa mwaka wote
wasinilipe, sitajali. Kama ningekuwa na makosa, ningerudi haraka sana na
kufuata wanachosema."
... akipishana na kocha wake Antonio Conte.
Costa anataka kurudi kwenye timu yake ya zamani ya
Atletico Madrid kwenye dirisha hili la usajili licha ya timu hiyo kufungiwa
kusajili hadi Januari mwakani.
Post a Comment