0


                 BARCELONA, HISPANI
CRISTIANO Ronaldo ameingia matatani. Ni baada ya kitendo chake cha kumsukuma Mwamuzi Ricardo De Burgos Bengoetxea katika mchezo ambao Real Madrid ilishinda mabao 3-1dhidi ya Barcelona na anaweza kufungiwa hadi michezo 12. 
Ronaldo alionyesha hamaki na kumsukuma mwamuzi huyo baada ya kutolewa nje kwa kadi ya pili ya njano, kutokana na kudaiwa kujiangusha ili kupata penalti alipokuwa akikabiliana na beki wa Barcelona, Samuel Umtiti.
Kwa kitendo cha kusukuma, Ronaldo anaweza kujikuta akitumikia kifungo hicho kirefu. Sheria za Hipsania zinasema mchezaji anaweza kufungiwa kati ya michezo minne hadi 12 kwa kumsukuma mwamuzi. 
Kifungo cha 96 cha sheria kinasema mchezaji atakayempora, kumsukuma na kumtingisha mwamuzi kwa dhumuni la kumfanyia kitendo cha kikatili atatumikia kifungo cha michezo 12 kwa kosa hilo.
Mwamuzi De Burgos Bengoetxea aliripoti tukio la kusumwa katika mchezo huo wa kwanza wa Super Cup wa Hispania, aliandika: “Mara baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu, moja kwa moja mchezaji alinisukuma na kuonyesha ishara ya kutokubaliana na maamuzi.” 

Ronaldo akimsukuma mwamuzi.
Straika wa Las Palmas, Marko Livaja alifungiwa michezo mitano ya La Liga kwa tukio kama hilo mwezi Aprili, mchezo mmoja kwa kadi nyekundu aliyoonyeshwa na mingine minne kwa kumsukuma mwamuzi.

...akipachika bao la pili.
Adhabu ya Livaja ilikuwa ni ya kutolewa mfano na Liga, kwa matukio ambayo hayapewi umuhimu yanayotokea mbele ya mwamuzi.
Bado kuna uwezekano wa Ronaldo kukata rufaa kwa kadi yake ya pili ya njano, lakini kwa adhabu yake ya kumsukuma mwamuzi itabaki kama ilivyo.

     ....akianguka baada ya kukumbanana Umtiti.
Nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos ameishauri klabu yake kukata rufaa kwa kadi ya pili ya Ronaldo na kudai mchezaji huyo hakuwa na nia ya kumdanyanya mwamuzi baada ya kuanguka kutokana na changamoto aliyoipata kutoka kwa beki Umtiti.
 “Nilikuwa mbali, lakini nadhani ilikuwa ni sehemu ya mchezo na kumfanya (Ronaldo) kupoteza balansi, bila ya kufanya kitu chochote,” Ramos alisema.
“Kumtoa nje mchezaji muhimu tunayemtegemea zikiwa zimebaki dakika 10 katika mchezo wa Al Clasico ni kitendo kilichotakiwa kufanyiwa tathimini na kufikiria sana.'  
Kocha wa Madrid, Zinedine Zidane pia alidokeza kuwa timu yake itakata rufaa, akitarajia kuwa na Ronaldo Jumatano katika mchezo wa marudiano utakaopigwa uwanjani Bernabeu.
“Tulicheza mpira mzuri sana, lakini kilichonikasirisha ni kutolewa kwa Cristiano Ronaldo,” Zidane aliwaambia waandishi. “Labda haikuwa penalti, lakini kutoa kadi nyekundu (kwa ushawishi) ilikuwa kitu kigumu.
“Hata hivyo, hatutaweza kubadilisha hilo, hata kama tutajaribu kuwa naye Jumatano.”
Kama Ronaldo atafungiwa mechi tano adhabu yake itahusisha pia mashindano yote ya Hispania ikiwemo Ligi Kuu ya La Liga.  Kama atafungiwa michezo minne au chini ya hiyo adhabu yake itakuwa katika michezo ya Super Cup ya Hispania tu.

...akionyeshwa kadi nyekundu
Ronaldo alipata kadi ya kwanza ya njano baada ya kufunga bao la pili la Madrid uwanjani Nou Camp kwa mkwaju wa mbali uliomshinda kipa wa Barcelona, Marc-Andre ter Stegen.
Baada ya kufunga bao hilo, straika huyo Mreno alivua jezi yake ya kuionyesha kwa mashabiki likiwa ni jibu la Lionel Messi aliposhangilia bao katika mchezo wa Al Clasico mwezi Aprili, Muargentina huyo alionyesha namba na jina lake kwa mashabiki uwanjani Bernabeu baada ya kufunga bao la ushindi dakika za mwishoni katika ushindi wa mabao 3-2. 
                  Messi Aprili baada ya kufunga bao la ushindi

Waamuzi wa Hispania hawajapanga kukutana hadi Jumatano, hapo ndipo watafamua uamuzi wa adhabu ya Ronaldo.  Madrid ilipata bao lake la kwanza baada ya beki Gerard Pique kujifunga kabla ya Messi kusawazisha kwa mkwaju wa penalti kufuatia penalti yenye utata ya Luis Suarez. 

Ronaldo akimjibu Messi 
Hata hivyo mabao ya Ronaldo aliyeingia kuchukua nafasi ya Karim Benzema na Marco Asensio yaliipa ushindi Madrid.  



Post a Comment

 
Top