MADRID, HISPANIA
CRISTIOANO RONALDO
amefungiwa michezo mitano baada ya kutolewa nje katika mchezo wa Super Cup
ambao timu yake ya Real Madrid ilishinda mabao 3-1dhidi ya Barcelona Jumapili
iliyopita.
Ronaldo amefungiwa
mechi moja kwa kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu na amefungiwa
mechi nne kwa kumsukuma mwamuzi kwa nyuma baada ya kutolewa nje.
Ronaldo alipata kadi
ya kwanza ya njano baada ya kuvua jezi yake wakati akishangilia bao alilofunga uwanjani
Nou Camp na kufanya matokeo kuwa 2-1.
Ronaldo mwenye umri
wa miaka 32, ana siku 10 za kukata rufaa na ataukosa mchezo wa marudiono wa
timu hizo utaopigwa uwanjani Bernabeu Jumatano.
Staa huyo wa
kimataifa wa Ureno anaweza kucheza michezo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini hataruhusiwa
kucheza mechi za Ligi ya La Liga hadi hadi Septemba 20 dhidi ya Real Betis.
Real Madrid
imeonyesha dalili za kukata rufaa kupinga kadi ya pili ya njano aliyopewa
Ronaldo kwa madai ya kujiangusha dakika 10 kabla mchezo huo kumalizika alipokuwa
akipambana na beki wa Barcelona, Samuel Umtiti.
"Kutolewa kwa Ronaldo
kumenishangaza kwasababu hata kama sio penalti, kadi ina ukakasi," alisema
bosi wa Madrid Zinedine Zidane baada ya mchezo.
"Tutaangalia kama tunaweza
kufanya kitu ili aweze kucheza Jumatano."
Ronaldo alidumu
uwanjani kwa dakika 24 baada ya kuingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya
Karim Benzema na alitolewa zikiwa zimesalia dakika 10 baada ya kuipa bao Madrid
na kuongoza 2-1.
Hii ni kadi nyekundu
ya 10 Ronaldo tangu ameanza kucheza soka
na kadi za njano za Jumapili zilikuja ndani ya dakika mbili.
Michezo ambayo Ronaldo ataikosa
|
Barcelona (nyumbani) – Hispania Super
Cup- 16 Agosti
|
Deportivo La Coruna (ugenini) - La
Liga - 20 Agosti
|
Valencia (nyumbani) - La Liga - 27
Agosti
|
Levante (nyumbani) - La Liga - 9 Septemba
|
Real Sociedad (ugenini) La Liga - 17
Septemba.
|
Post a Comment