BARCELONA,
HISPANIA
NEYMAR yuko
mbioni kufanyiwa vipimo na Klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) wiki hii, kwa
mujibu wa ripoti.
Nyota huyo wa Barcelona anadaiwa
kukubaliana maslahi binafsi na miamba hiyo ya Ufaransa na kufanya uhamisho wa
kushtua wa Pauni 196 milioni.
Neymar hajaambatana
na kikosi cha timu yake kurudi Barcelona kutoka Miami katika ratiba ya
maandalizi ya msimu mpya.
Staa huyo ameenda China
kutika ziara ya mdhamini, na akitoka huko atasimama Qatar ambapo atakutana na
Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi.
Gazeti la Qatari la Al
Watan limeripoti kuwa, Neymar mwenye umri wa miaka 25-atasafiri kwenda nchini
humo kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya katika siku za hivi karibuni kwa
ajili ya kujiunga na PSG.
Imeripotiwa kundi la
matajiri kampuni ya uwekezaji wa michezo wa Qatari ambao ndio wanaoimiliki wa
PSG, wamempa ofa Mbrazili huyo ya Pauni 270 milioni.
Neymar aliondoka na baba yake ambaye pia ni wakala wake.
Magazeti ya Hispania
yamasema kiasi hicho cha pesa kitakuwa ni malipo yake ya kuwa balozi wa Qatar
katika Kombe la Dunia mwaka 2022 yatakayofanyika Qatari.
Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi.
Lakini pia inadaiwa
kiasi hicho kitatumika kulipia ada yake ya uhamisho kwa mujibu kifungu
kilichomo katika mkataba wake na kulazimisha kuhamia Ligue 1.
Post a Comment