0


                    LONDON, ENGLAND
DIEGO COSTA (pichani chini) ameendeleza vita yake na Chelsea baada ya kukataa ombi la klabu hiyo la kurudi kikosini na kusema asingeweza kukatisha ziara yake ya Brazil. 
Straika Costa kwa sasa yuko nyumbani kwao alikokulia, Lagarto, baada ya Kocha wa Chelsea, Antonio Conte kumwambia kupitia ujumbe wa simu (SMS) kuwa hayumo katika mipango yake msimu huu. 
Pia, Costa amedai Chelsea itamlazimisha kufanya mazoezi na wachezaji wa akiba kama atarudi klabuni hapo.
Hivi karibuni Chelsea ilitangaza kumpkiga faini ya Pauni 300,000 na atakatwa zaidi kama hatarudi London. 
Klabu ya Atletico Madrid inaweza kumlipa Costa pesa anazokatwa kama dili la kumnasa linaweza kumalizika kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili la majira ya joto.

Tatizo kubwa, Atletico Madrid imefungiwa kusajili hadi katika dirisho dogo la Ulaya litakalofungiwa Januari. Inachoweza kufanya ni kumsajili na kutoa kwa mkopo.
Aidha Costa aliweka wazi mpango wake wa kukaa hadi mkataba wake utakapoisha Chelsea ili aondoke bure.­ 
Chelsea ilimtaka straika huyo wa kimataifa wa Hispania mwenye asili ya Brazil kurudi kundini lakini Alhamisi Costa aliikana klabu hiyo hadharani.
Baada ya kufanya mkutano na Chama cha Soka cha Sergipe, Kaskazini Mashariki mwa Brazil, Costa alisema: “Nimeshafanya uamuzi wangu wapi ninakoelekea. Napaswa kurudi Atletico Madrid.
                          Nataka kurudi Atletico Madrid

“Kuna mgogoro, inaonekana kama Chelsea haitaki kuniruhusu kuondoka. Lakini ninaamini hali hii itamalizika sasa ninaporudi Hispania.” 
Costa alisema: “Nimeshasema kama kocha hanitaki, timu ninayotaka kwenda ni Atletico Madrid."
“Nimekataa ofa nyingine nyingi tu. Wao wanataka kuniuza China au klabu nyingine. Kama nitaondoka, ninataka kujiunga na klabu ninayotaka- siyo klabu inayolipa zaidi.
“Ninataka dili na Atletico limalizwe ndani ya mwezi huu. Mawazo yangu ni kwenda Madrid, kufanya mazoezi pale na kujiweka katika hali nzuri na kuwa tayari kukiwasha katika Kombe la Dunia linalokuja.

“(Diego) Simeone ananitaka. HiIo liko wazi sana. Nimekuwa na dhamana naye. Mashabiki na watu wananipenda pale. Wananiheshimu. Wananitazama kama binaadamu na mchezaji wa soka.”

Post a Comment

 
Top