NEYMAR ameanza kuweka
alama zake klabuni Paris Saint-Germain (PSG) baada ya kufunga bao moja na
kuasisti lingine katika ushindi wa mchezo wa Ligue 1 dhidi ya Guingamp.
Straika huyo wa
kimataifa wa Brazil, huo ulikuwa mchezo wake wa kwanza akiitumikia PSG tangu
alijiunga akitokea Barcelona kwa uhamisho dau la rekodi ya dunia Pauni 198 milioni.
Neymar amefungua
akaunti yake ya mabao katika dakika 82 akipokea pasi kutoka kwa Edinson Cavani.
Mapema katika dakika ya 62, Neymar alitengeneza pasi
ambayo Cavani aliikwamisha wavuni.
Mchezaji huyo ghali
zaidi duniani pia alihusika katika kutengeneza bao la kwanza katika dakika 52
la kujifunga la beki wa zamani wa PSG, Jordan Ikoko akiwa anamtengenezea nafasi
Cavani.
Neymar alianzia
upande wa kushoto akiwa na mastaa wengine Cavani na Angel di Maria ambao
walikuwa moto dhidi ya timu pinzani.
Post a Comment