MERSEYSIDE, ENGLAND
WAYNE ROONEY ‘Wazza’ ameondoka Manchester United na kujiunga tena na timu yake ya zamani ya Everton kwa ada ambayo mpaka sasa haijwekwa wazi.
Staa huyo mwenye umri wa miaka 31- ameingia mkataba wa miaka miwili Goodison Park baada ya kuondoka Old Trafford.
Katika waraka wake, Rooney alisema: "Ni muda sasa tangu niliposema klabu ninayotaka kuichezea katika Ligi Kuu England zaidi ya Manchester United ni Everton, kwa hiyo nina furaha kwa jambo hilo kutokea.
"Miaka 13 iliyopita nilienda United kwa lengo la kushinda mataji na nina furaha kuwa sehemu ya mafanikio makubwa katika nyakati za historia ya klabu hiyo.
"Nimerudi Everton kwa sababu ninaamini Ronald Koeman (kocha) anatengeneza timu ambayo inaweza kushinda kitu na ninataka kuwa sehemu ya jambo hilo katika klabu ambayo nimekuwa nikiishabikia tangu utotoni."
Kocha wa Everton, Ronald Koeman aliuambia mtandao wa klabu hiyo: "Wayne amenionyesha ari tunayoihitaji na tabia ya ushindi aliyonayo na mtazamo wake wa ushindi- anajua jinsi ya kushinda mataji na ninafurahi ameamua kuja hapa.
"Anaipenda Everton na alikuwa na hamu ya kurudi hapa. Ana umri wa miaka 31 na sina wasiwasi kutokana na kiwango chake. Atafanya maajabu hapa."
Rooney akikabidhiwa jezi na kocha wake, Koeman.
Mwaka 2004, Rooney alijiunga na United, aliondoka Everton akiwa na umri wa miaka 18- kwa dili la Pauni 25.6 milioni.
Akiwa na United alifunga mabao 253 katika michezo 559, akishinda taji la Ligi Kuu England mara tano.
Januari mwaka huu alifunga bao lake la 250 akiwa United akivunja rekodi iliyowekwa na Sir Bobby Charlton.
Rooney aliondoka Everton miaka 13 iliyopita.
Rooney ni mchezaji wa tano wa kucheza michezo mingi kwa muda wote, pia ameshinda mataji ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Europa League, Kombe la FA na mataji matatu ya Kombe la Ligi ndani ya misimu 13 alipokuwa akiitumikia timu hiyo.
Alichaguliwa kuwa nahodha wa United na kocha wa zamani, Louis van Gaal mwaka 2014 kufuatia kuondoka kwa Nemanja Vidic aliyejiunga na Inter Milan.
Kocha wa United, Jose Mourinho aliuambia mtandao wa klabu hiyo: " Siyo siri, kwa kitambo kirefu nimekuwa nikivutiwa na Wayne. Amekuwa mchezaji wa kimataifa muda wote alipokuwa klabuni na atabaki katika historia ya vitabu kwa miaka mingi ijayo.
Mazoezini na wachezaji wenzake
"Sio rahisi kumuona mchezaji
mkubwa kama yeye kukubali kuichezea klabu ya chini na aliyokuwa awali na
sikukubaliana naye aliponiambia anataka kurudi Everton. Uzoefu wake, mtazamo na
matamanio vitakosekana klabuni Man United na namtakia mafanikio."Rooney alianza kupoteza uwezo wake uwanjani akiwa na Man United msimu uliopita na alianza katika michezo 15 ya Ligi Kuu England.
Awali alitajwa kwenda kujiunga na timu za Ligi Kuu ya China na ile ya Marekani, lakini siku zote ilikuwa dhahiri kama angeondoka United, angerudi Everton mara nyingi ameonekana kuipenda klabu hiyo.
Mtendaji Mkuu wa United, Ed Woodward alisema: "Wayne alikuwa mtumishi wa ajabu alipokuwa na United, tangu alipojiunga nasi akiwa kijana mwenye kipaji, alikuwa sawa na mlipuko kwa misimu yote13.
"Nani anaweza kusahau mabao yake matatu ‘hat-trick’ dhidi ya Fenerbahce, alifanya kitu cha kushangaza dhidi ya Man City na amefanya mengi yasiyohesabika. Lakini baada ya mazungumzo ya muda, klabu ilikubaliana na uamuzi wake wa kujiunga na timu yake ya utotoni.
Rooney akijifua
"Anakwenda kutengeneza kitu kingine katika historia ya klabu. Wayne anaondoka kwetu akiwa mfungaji wa muda wote na ameshinda kila taji kubwa.
"Rekodi yake itachukua zaidi ya miaka 10 kwa mtu mwingine kuifikia na nina furaha kwa jinsi alivyokuwa mstari wa mbele tangu alipochaguliwa kuwa nahodha wa timu miaka mitatu iliyopita.
“Kwa niaba klabu na mashabiki wetu zaidi ya mamilioni duniani kote, tunamtakia Wayne awamu nyingine bora ya kazi yake ya kuvutia."
Everton imetangaza Rooney atavaa jezi No. 10, kufuata nyayo za shujaa wake wa utotoni, Duncan Ferguson ambaye alivaa namba hiyo aliporejea kwa mara ya pili.
Kuondoka Rooney kutoka Everton miaka 13 iliyopita kuliwafanya baadhi ya mashabiki kupandwa na hasira, lakini mchezaji huyo hajawahi kuikana asili yake na amekuwa akikaririwa akizungumzia mapenzi yake na klabu hiyo ya Merseyside.
akiwa na wachezaji wenzake
Alipokuwa akitumikia Man United alivaa
fulana ya ndani iliyoonyesha mapenzi yake kwa Everton, na aliichezea timu hiyo
tena wakati Duncan Ferguson alipostaafu mwaka 2015.Rooney ambaye anashikiria rekodi ya ufungaji ya Timu ya Taifa ya England amejiunga Everton na wachezaji wengine wapya kina Jordan Pickford, Davy Klaassen, Michael Keane, Henry Onyekuru, Nathangelo Markelo na Sandro Ramirez.
Post a Comment