MANCHESTER, ENGLAND
JOSE MOURINHO anakaribia
kukamilisha dili la Pauni 75 milioni kumnyakua straika wa Everton, Romelu
Lukaku na kuiacha Chelsea katika mataa.
Lukaku mwenye umri wa
miaka 24, anatarajiwa kufanyiwa vipimo katika kituo cha afya cha kampasi ya
UCLA mjini California na kuachana rasmi na Everton.
Everton imekasirishwa na
kitendo cha straika huyo aliyefunga mabao 25 msimu uliopita kukwepa kuhudhuria
maandalizi ya msimu ujao na timu hiyo.
Kocha wa Everton, Ronald
Koeman alionekana kuchukizwa zaidi baada ya kumpigia simu staa huyo na
kutopatikana.
Bosi wa Old Trafford,
Mourinho anamnyakua staa huyo wa kimataifa wa Ubelgiji baada ya kuwazidi ujanja
wapinzani wake wa Ligi Kuu, Chelsea- na straika huyo amekubali dili la miaka
mitano na mshahara wa Pauni 250,000 kwa wiki.
Chelsea inaamini
ilichelewa kufanya uamuzi Alhamisi asubuhi wakati Lukaku alipokubali kwa moyo
wake wote kurejea Stamford Bridge.
Lukaku
Mabingwa hao watetezi wa
Ligi Kuu walikuwa wanasubiri kukubaliwa kwa ofa ya kuondoka kwa straika wao,
Diego Costa kabla ya hawajamalizana na Lukaku.
Lakini timu hiyo ya
London iliachwa katika mshangao kwa kitendo cha Mourinho kuwafanyia umafia na
kumchukua straika huyo.
Lukaku ambaye kwa sasa
yupo mapumzikoni jijini Los Angeles akiwa na staa wa Man United, Paul Pogba,
atakuwa kati ya wachezaji wanne ghali wa soka duniani.
Inafahamika kwamba Pogba
ndiye aliyemshawishi Lukaku kuachana na mpango wa kurudi Chelsea.
Kwa mujibu wa habari za
ndani za Manchester United, staa huyo anatarajiwa kuvaa jezi No 9 iliyookuwa ikivaliwa na Zlatan Ibrahimovic.
Pogba na Lukaku
United ilibadilisha
mwelekeo na kumnasa Lukaku baada ya Real Madrid kukataa kupunguza dau la Pauni
85 milioni kwa ajili ya straika wa Kihispania, Alvaro Morata.
Dili la Lukaku
halihusiani na lile la0 Wayne Rooney kurudi Goodison Park (Everton) baada ya
kuondoka miaka 13 na kujiunga na United.
Rooney ataruhusiwa kuondoka kwa uhamisho wa bure.
Mambo safi: Jose Mourinho
Dili hili linatarajiwa
kufanyika haraka, na staa huyo mwenye umri wa miaka 31- tayari amekubali
kushusha mshahara wake kurudi katika klabu yake ya hiyo ya kwanza kuitumikia.
Kama ataendelea kubaki
United, Roney atakuwa akivuna Pauni
300,000 kwa wiki msimu huu wakati
Everton haiwezi kumlipa Zaidi ya Pauni160,000 kwa wiki.
Kocha Koeman akiwa na Lukaku
Kwa bosi wa Chelsea,
Antonio Conte, kumkosa mchezaji huyo aliyekuwa na uhakika wa kumrudisha
Stamford Bridge kutaongeza hasira zake za kuwakosa wachezaji aliopanga kuwanasa
katika mipango yake ya msimu ujao.
Pogba akiwa na Lukaku jijini Los Angelese, Marekani.
Hata hivyo, Lukaku bado
ana hasira dhidi ya Mourinho, ambaye alimuuza kutoka Chelsea kwenda Everton
mwaka 2014 kwa dau la Pauni 28 milioni.
Post a Comment