0



LONDON, ENGLAND
DIEGO COSTA amezuiwa kujiunga na Chelsea katika maandalizi ya msimu mpya wakati huu akiwa mbioni kukamilisha uhamisho wake wa kurudi katika timu yake ya zamani ya Altetico Madrid.
Kocha Antonio Conte na wachezaji wake waliotwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu uliopita walitarajiwa kuripoti katika viwanja vya mazoezi vya Surrey Jumatatu wiki hii.
Wawakilishi wa Costa wamekubali kuendelea kwa mapumziko ya straika huyo katika majira haya ya joto wakati wakiendelea na mipango ya kumuondoa Stamford Bridge.
Klabu za Atletico na Chelsea zinapaswa kukubaliana thamani ya staa huyo wa kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 28- aliyebakisha miaka miwili katika mkataba wake Chelsea.
Mazungumzo yataendelea, ingawaje ugumu upo kwa Atletico ambayo hairuhusiwi kusajili wachezaji wapya hadi dirisha la Januari.
Lengo la Altetico na kumnunua na kumtoa kwa mkopo katika klabu nyingine na kumchukua  Januari.

Costa baada ya kupachika bao
Costa anataka kuondoka Chelsea na Kocha Conte hamtaki staa huyo. Uhusiano binafsi kati ya wawili hao umevunjika.
Kocha Conte alimtumia ujumbe Costa mwishoni mwa msimu ulioisha na kumtakia afya njema na kumtaarifu kuwa hakuwa katika sehemu ya mipango yake msimu ujao.
Costa alichukizwa na kitendo hicho na kuutoa ujumbe huo hadharani huku akiweka msimamo wa kutojiunga na klabu nyingine zaidi ya Atletico Madrid, ambayo ilimuuza Chelsea kwa dau la Pauni 32 millioni mwaka 2014.

  ...alikuwa mfungaji bora wa Chelsea msimu uliopita.
Pamoja na Manchester United kumnyakuwa Romelo Lukaku aliyekuwa akiwindwa Chelsea lakini bado hakuna mwafaka uliofikiwa kwa pande mbili hizo.
Kocha Conte anayevutana na suala la usajili na viongozi wa Chelsea anategemea kuwapo kwa mabadiliko kabla ya timu hiyo kwenda katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya China na Singapore wiki ijayo.

...anachotaka ni kurudi Atletico Madrid tu.
Kiungo Eden Hazard, aliyekuwa akifanya vizuri wakati Costa alipokuwa nje msimu uliopita, ni majeruhi na Michy Batshuayi  hana uhakika na maisha yake ya baadaye klabuni hapo.
Batshauyi alifunga bao lililoipa ubingwa timu hiyo msimu uliopita, ameonekana kuwa mchezaji wa kawaida na amekubali kuondoka.

....aliiweka hadharani meseji ya Conte.
Chelsea itarudi katika lengo lake la kuwanasa Alvaro Morata wa Real Madrid na straika wa Torino ya Italia, Andrea Belotti.  


Post a Comment

 
Top