0


              HOUSTON, MAREKANI
MANCHESTER UNITED imemongeza matumaini yake ya kumnasa winga, Gareth Bale (pichani chini) baada ya Bosi wa Real Madrid, Zinedine Zidane kukiri kuwa hana uhakika kama nyota huyo ataendelea kuwepo Bernabeu msimu ujao.
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ni shabiki mkubwa nyota huyo wa kimataifa wa Wales, na United bado inahitaji kuongeza wachezaji wengine katika kikosi chake.
Akizungumza baada ya kushuhudia kikosi chake kikichapwa mabao 4-1 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Manchester City uliofanyika Marekani, Zidane ameonyesha wasiwasi juu ya maisha ya baadaye ya Bale kikosini humo, kama ilivyo kwa Cristiano Ronaldo na Karim Benzema.
Bosi huyo Mfaransa alisema: “Nina matumaini BBC (Benzema, Bale na Cristiano) itabaki kwa msimu huu. Nina imani kila mtu atabaki. Ninataka kila mmoja aliyepo hapa abaki. Lakini lolote linaweza kutokea hadi kufikia Agosti 31.”
United ilifanya jaribio lake la kwanza kumnasa Bale mwaka 2007, lakini akiwa mchezaji wa Southampton aliamua kujiunga na Spurs. Mwaka 2013 United ilijaribu tena kumnasa staa huyo wa Wales lakini safari hii aliangukia katika mikono ya Real Madrid katika usajili uliovunja rekodi ya dunia.
Ningependa kila mtu angebaki.
Hii itakuwa mara ya tatu kwa Mashetani Wekundu kujaribu bahati yao- na wanaweza kufanikiwa kama Madrid itamnasa staa wa Monaco, Kylian Mbappe.

Mbappe ndiye atakayeamua hatma ya Bale
Mabingwa hao wa La Liga wameonyesha nia ya kumchukua kinda huyo wa Monaco mwenye umri wa miaka 18, na wameweka rekodi ya dunia ya Pauni161 milioni.
Usajili huo unaweza kutishia uwepo wa Bale-Benzema-Ronaldo Real Madrid, hilo linampa matumaini mapya Mourinho na United kwamba sasa wanaweza kumpata mtu wao.

Post a Comment

 
Top