0


                      LONDON, ENGLAND
MADAKTARI wa Arsenal wamesafiri hadi Chile kumwangalia Alexis Sanchez na kuthibisha kuwa anaugua mafua, na kuwaondoa hofu mashabiki waliouona ujumbe wake katika mitandano ya kijamii akidai ni mgonjwa.
Bosi Arsene Wenger alimpa mapumziko staa huyo wa kimataifa wa Chile, amesisitiza kwa mara nyingine kuwa hataondoka Emirates msimu huu.
“Anaugua mafua. Nilipata ujumbe wake (SMS) jana (Ijumaa), atarudi haraka iwezekanavyo. Tunawasilina naye pamoja na madaktari wake. Hakuna tatizo kubwa isipokuwa alipaswa kurudi kesho (Jumapili) lakini sasa atarudi Jumanne,” alisema Wenger Jumamosi.
Sanchez mwenye umri wa miaka, 28, aliposti picha katika mitandao ya kijamii akiwa sambamba na mbwa wake na kusindikiza na ujumbe: “Naumwa nikiwa katika mapumziko ya Kombe la Mabara.”
Inafahamika kuwa nyota huyo anataka kucheza katika klabu inayoshiriki Ligi ya Mabingwa lakini pamoja na Manchester City kuonyesha kumhitaji, Kocha Wenger amesisitiza kuwa hatauzwa, pamoja na kubakiza mwaka mmoja tu katika mkataba wake.
“Hakuna maendeleo zaidi, yako vilevile tu. Anabaki, bila shaka,” alisema Wenger.

Sanchez: Naumwa
Alipoulizwa kama Sanchez amewahi kumwambia kuwa anataka kuondoka, Wenger aliongeza: “Siwezi kuweka wazi alichokisema, siwezi kuvujisha siri ya mazungumzo yetu.”
Man City imesema ina uhakika Sanchez atajiunga nao, lakini Mtendaji Mkuu wa Arsenal, Ivan Gazidis ameahidi katika majira haya ya joto kutakuwa na kichocheo cha mabadiliko.
Kocha Wenger na Bodi ya Arsenal wanakubaliana kuwa wanahitaji kubaki na Sanchez, hata kama mkataba wake wa sasa unaelekea ukingoni.

Wenger: Haondoki ng'o
Sababu kubwa ya Wenger kumzuia mchezaji huyo ni rekodi yake ya mabao 30 na asisti 19 msimu uliopita anaamini pengo lake halina mbadala na ndoto ya muda mrefu ya Arsenal kushindania ubingwa haitaweza kutimia, hakuna mchezaji anayeweza kuweka takwimu kama zake.

                Lemar (kushoto) anaweza kuwa mbadala wake
Hata hivyo, bado Arsenal haijakata tamaa kumsajili nyota wa Monaco, Thomas Lemar- ingawaje pamoja na kwamba anaweza kuvunja rekodi ya klabu hiyo ya ada ya Pauni 60 milioni mpaka kumpata.
Tayari Monaco imeshawauza Bernardo Silva na Benjamin Mendy kwenda Manchester City kwa jumla ya dau la Pauni 90 milioni na Tiemoue Bakayoko kwenda Chelsea kwa Pauni 34 milioni.

anataka kucheza Ligi ya Mabingwa.
Real Madrid iko tayari kulipa Pauni 160 milioni kumnasa kinda mwenye umri wa miaka 18, Kylian Mbappe.  Arsenal inaamini kama dili hilo litafanikiwa, ndoto yao ya kumsana Lemar itakuwa imefikia ukingoni­­­­­­.

Post a Comment

 
Top