MANCHESTER, ENGLAND
ERIC BAILY (pichani juu) wa Manchester
United amefungiwa mechi tatu baada ya kupata kadi nyekundu katika mchezo wa
Europe League dhidi ya Celta Vigo.
Beki huyo wa kati
mwenye umri wa miaka 23- alitolewa nje baada ya kurusha ngumi katika mchezo wa
nusu fainali uliochezwa Mei 11 na akakosa fainali dhidi ya Ajax, ambayo United
ilishinda mabao 2-0.
Hata hivyo, adhabu
imeongezwa na sasa atatumikia mechi mbili zaidi.
Kwa maana hiyo, Bailly
ataukosa mchezdo wa Super Cup dhidi ya Real Madrid utakaopigwa Agosti 8 na
mchezo wa kwanza wa makundi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Beki huyo wa
kimataifa wa Ivory Coast kesi yake haiwezi kukatiwa rufaa kwa sababu bodi ya
Uefa hufanya uamuzi kutokana na kile kilichoamuliwa na mwamuzi.
Bailly alitolewa kwa
kitendo chake cha kumrushia ngumi mchezaji wa Celta Virgo ambaye aliwahi kuitumikia Manchester
City, straika, John Guidetti. Na mchezaji wa Celta Virgo, Facundo Roncaglia alitolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo huo kwa kosa la
kurudishia.
Manchester United pia
ilipokea onyo kali kutoka Uefa kwa kosa hilo.
Post a Comment