0


                     HOUSTON, MAREKANI
ROMELU LUKAKU na Marcus Rashford wameichinja Manchester City baada ya Manchester United kushinda mchezo wa kwanza wa derby katika ardhi ya ugenini.
Lukaku alikuwa wa kwanza kupachika bao katika dakika ya 37 likiwa ni bao lake la pili tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea Everton wiki iliyopita.
Raia huyo wa kimataifa wa Ubelgiji alifunga bao la kuvutia baada ya kumalizia mpira uliopigwa katikati ya uwanja na kwenda pembeni ya lango   alipomzidi maarifa kipa mpya wa Man City, Ederson aliyenuniliwa kwa Pauni 35 milioni.
Dakika mbili baadaye, Rashford alipokea pasi kutoka kwa Henrikh Mkhitaryan akiwa peke yake upande wa kulia wa eneo la penalti la Man City na kumfunga kipa Ederson kuihakikishia ushindi timu yake.
Ushirikiano wa Lukaku na Rashford unaifanya United kuwa na matumaini ya kufanya vizuri msimu ujao wa Ligi Kuu baada ya kutengeneza nafasi nyingi dhidi ya City, ambao walikuwa wakicheza mchezo wao wa kwanza ya matayarisho ya msimu.

...wakishangilia bao la kwanza
Lukaku alikosa nafasi mbili za wazi kipindi cha pili, akikosi kwa kichwa kufuatia kona iliyopigwa na Rashford na kugonga nguzo ya goli baada ya kuachia shuti kali kwa mguu wa kushoto.
"Siwezi kuwa na furaha zaidi ya kile alichokifanya, na siwezi kuwa na furaha kwa kuwa tumemsajili kabla ya kuanzia kwa msimu," Kocha wa United Jose Mourinho alisema kuhusu Lukaku kupitia Televisheni ya klabu hiyo (MUTV). 

                      Mourinho raha tele upande wake.
"Ni mchezaji anayecheza kitimu, anayezuia mpira, anayesubiri msaada, anayeruhusu timu kuondoka eneo la presha. Watu wanaangalia mabao na nafasi, binafsi nina mtazamo tofauti," aliongeza Mourinho.

Post a Comment

 
Top