0


                   HONG KONG, CHINA
 JURGEN KLOPP ametuma ujumbe mzito kwa Barcelona baada ya kuimbia kuwa Philippe Coutinho hauzwi.  Bosi huyo wa Anfield ameikataa ofa dau la Pauni 72 milioni iliyotolewa na miamba hiyo ya Catalunya.
Akizungumza baada ya kumshuhudia mchezaji huyo raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 25- akifunga bao la ushindi katika mchezo wa Kombe la Ligi Kuu la barani Asia dhidi ya Leicester, Klopp alisema ana kauli ya mwisho kuhusu nyota huyo.
“Kama nasema hauzwi, hauziwi,” alifafanua. “Hakuna jambo lingine la kuongeza. Ni uamuzi wa klabu, ni uamuzi wangu. Hivyo ndivyo ilivyo.”
Alipoulizwa kama Bodi ya Liverpool imemhakikishia kuwa Coutinho hatauzwa, Klopp alijibu: “Ninaweza kusema mara 20, hauzwi. Kama unaulizwa swali lkwa njia nyingine nasema, hakuna uhakika, unaitengeneza stori katika mtindo mwingine. Hakuna stori kwangu. Lolote litakalotokea upande wao, nasema hauzwi. Jibu ni hauzwi.”
Barcelona, inayojipanga kupata Euro 222 milioni (Pauni199 milioni) na kuvunja rekodi ya dunia kwa uhamisho wa Neymar kwenda Paris Saint-Germain,  imeijaribu kuipima Liverpool kwa dau la Pauni 75 milioni kama ililolipa kwa Luis Suarez mwaka 2014.

Coutinho
Lakini Klopp, ambaye alishudia Liverpool ikimpoteza Raheem Sterling kwenda Manchester City mwaka 2015 alipowasili Merseyside, alisema mambo yamebadilika.
“Kwa Suarez nilikuwa mbali,” alisema kocha huyo wa zamani wa Borussia Dortmund. “Pindi klabu ilipomuuza Sterling Iabda nilikuwa mtu wa mwisho kujua. Pia, ishu hizo hazihusiana na hii. Tunakaribia wakati muhimu na tunataka kuwa bora.
Tunahitaji kubaki na wachezaji wetu nyota. Hilo ndio jibu.”
Usiku wa Ijumaa, Klopp alizungumza na Coutinho katika Hoteli ya Ritz Carlton, ambako Liverpool imefikia katika ziara yake ya Hong Kong. Lakini alipoulizwa kilichozungumza alijibu: “Sio kwa ajili yako.”

Pia, Klopp aliongeza Coutinho, aliyesaini dili la kuitumikia timu hiyo hadi mwaka 2022, ana furaha Merseyside.

                                    Sina mpango wa kumuuza Coutinho
“Kila mmoja anajua Phil Coutinho ni mchezaji muhumu kwetu,” alisema. “Najua anahisi zaidi ya furaha, ameridhika- jijini Liverpool. Anaipenda klabu na mji- hiyo iko wazi.”

Post a Comment

 
Top