BEIJING, CHINA
ANTONIO CONTE amefunguka kwa mara ya
kwanza tangu alipodaiwa kumtumia ujumbe wa kumtaarifu kutokuwa katika mipango
yake ya msimu ujao straika, Diego Costa mwishoni mwa msimu uliopita.
Mwezi uliopita Gazeti
la Hispania AS lilidai liliona Ujumbe Mfupi wa Maneno (SMS) ambao
ulikuwa ukimfahamisha Costa kuwa hatakuwa sehemu ya wachezaji wa Ligi Kuu upande
wa Chelsea msimu ujao.
Kwa mujibu wa gazeti
hilo, ujumbe wote uliotoka kwa Conte ulisomeka hivi: “Hi Diego, nadhani
unaendelea vizuri. Asante kwa msimu mzuri tuliokuwa pamoja. Kila la heri kwa
mwaka ujao lakini hutakuwa katika mipango yangu msimu ujao.”
“Mimi ni mchezaji wa Chelsea, lakini
hawanitaki,” Costa alikaririwa akiwaambia waandishi wa habari baada ya kuitumikia
Timu ya Taifa ya Hispania.
Hata hivyo, Conte amevunja
ukimya kuhusu suala hilo na kudai Costa na wakala wake walishaambiwa miezi sita
iliyopita kuwa nyota huyo ataondoka katika usajili wa majira ya joto.
Inadaiwa kuwa Chelsea iliamua kuachana
na Costa baada ya kutaka kufuata pesa nyingi katika Ligi Kuu ya China kujiunga
na klabu ya Tianjin Quanjin.
Chelsea ilizuia uhamisho huo lakini
uamuzi uliofanywa na Conte baada ya hapo hakuna jinsi ya kuubadilisha.
“Sipendi kuwazungumzia wachezaji ambao
hawapo hapa,” alisema Conte, kwa mara ya kwanza tangu zilipozagaa taarifa za
kumtumia ujumbe Costa
Enzi za uswahiba wao ndani ya Chelsea.
“Januari, suala la Costa liliwekwa wazi.
Kwa klabu, kwake na wakala wake na mimi na likafungwa.”
Costa alikuwa mfungaji bora wa msimu
kwa kupachika mabao 20 katika Ligi Kuu na Chelsea ikatwaa taji.
Anataka kurudi katika timu yake ya
zamani ya Atletico Madrid na amepewa mapumziko ya ziada ili kukamilisha
uhamisho wake katika usajili huu wa majira ya joto.
Baada ya kumkosa Romelu Lukaku
aliyejiunga na Manchester United kwa dau la Pauni 90 milioni, Chelsea imemsajili
Alvaro Morata kuziba pengo lake.
... safi sana Conte akimpongeza Costa
Morata,
alifanyiwa vipimo vya afya jijini London Alhamisi atavunja rekodi ya usajili ya
klabu hiyo inayotakiwa kutoa Pauni 58 milioni na inaweza kupanda hadi kufikia
Pauni 70 milioni.
Post a Comment