LOS
ANGELES, MAREKANI
MANCHESTER
UNITED imefanya usajili wake wa pili katika
msimu huu wa majira ya joto kwa kuvunja rekodi na kumnasa Romelu Lukaku – kuhitimisha
furaha ya Kocha Jose Mourinho aliyewashinda waajiri wake wa zamani, Chelsea.
Lukaku mwenye umri wa
miaka 24- ametua Old Trafford kwa ada ya uhamisho ya Pauni 75 milioni- na
kumfanya kuwa straika ghari zaidi katika historia ya soka la Kiingereza.
Staa huyo wa
kimataifa wa Ubelgiji ameingia dili la miaka mitano, lenye thamani Pauni 200,000-kwa
wiki na uwezekano wa kuongeza mwaka mwingine zaidi.
Atavaa jezi No 9 iliyokuwa
ikivaliwa na Zlatan Ibrahimovic msimu uliopita.
Lukaku alikuwa
akiwaniwa na klabu mbili za United na klabu yake ya zamani ya Chelsea ili kutoa
huduma yake na uamuzi wake umekuwa pigo kubwa kwa mabingwa watetezi, Chelsea.
Post a Comment