MADRID, HISPANIA
RAIS wa Barcelona, Josep Bartomeu amekiri kumchemsha
kumshawishi supastaa Mbrazili, Neymar (pichani juu) kubaki klabuni hapo, akawaomba mastaa,
Lionel Messi na Luis Suarez wajaribu kumtuliza.
Habari
kutoka Hispania zinadai, Messi na Suarez wamezungumza na Neymar wakiwa katika
maandalizi ya msimu jijini New Jersey na pia Gerard Pique ameongeza nguvu
kumshawishi staa huyo kubaki Nou Camp.
Hali hiyo imekuja
baada ya Rais Bartomeu kuwaambia waandishi wa habari Barcelona inakuwa na utulivu
kuhusu ripoti za kutaka kumpoteza staa wake namba mbili katika usajili huu wa
majira ya joto.
Katika hali isiyotarajiwa nyota wa mahasimu wao Real Madrid, Cristiano
Ronaldo naye amemwambia Neymar aachane na mpango wa kutua
Paris Saint-Germain (PSG).
Ronaldo
alisema amefanya mawasiliano na Neymar na kumwambia atafanya makosa kama atajiunga
na miamba hiyo ya Ufaransa. Mchezaji
huyo bora a dunia amemwambia Mbrazili huyo ni bora atue Manchester United kama atakuwa
tayari kuondoka Nou Camp.
... akiwa kazini
Mbali
na upinzani ndani ya uwanja, Ronaldo na Neymar ni marafiki wa karibu na urafiki
wao umeongezeka kutokana na wote kudhaminiwa na Kampuni ya Nike.
akiwa na Suarez na Messi
Baadhi
ya magazeti ya Hispania yameripoti wawili hao wamekuwa wakijadiliana kuhusu suala
hilo la Neymar kutaka kutua PSG kwa dau la Pauni 195 milioni.
Imedaiwa
Ronaldo (pichani juu) amemtumia ujumbe wa WhatsApp akimuonya Neymar (25) kuhusu hatua yake ya
kutaka kuachana na La Liga kwa ajili ya Ligue 1.
PSG
imeahidi kumlipa Neymar Pauni 500,000 kwa wiki akijiunga na timu yao- na klabu
hiyo ina mipango ya kutumia usajili huo
kujitangaza duniani.
Neymar, Messi na Ronaldo.
Lakini
Ronaldo amemwambia Neymar atapiga hatua nyuma kama atang’ang’ania uamuzi wake
wa kucheza ligi nyepesi na kujiunga na klabu ndogo.
Mchezaji
huyo bora wa mwaka anaamini ni klabu za Real
Madrid, Manchester United au Barca ndizo zinaweza kumpandisha hadhi Neymar
duniani. Na
akamwambia Neymar kama ana hamu ya kuondoka Nou Camp ni bora aende Old Trafford
kwa sababu ina kuongeza thamani ya picha zake duniani.
.... amemwambia Rais Bartomeu anataka kuondoka
Neymar kwa
sasa yuko Marekani akiwa na Barcelona katika ziara ya michezo ya kujiandaa na
msimu mpya, na alifunga mabao yote katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya
Juventus usiku wa Jumamosi jijini New York.
Straika
huyo Mbrazili alifanya mkutano na Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu Ijumaa
iliyopita na kuwasilisha madai yake ya kutaka kuondoka klabuni hapo.
akionyesha umuhimu wake dhidi ya Juve.
Inadaiwa
Rais Bartomeu alimsihi nyota huyo asiondoke na kumpa muda ili kuweka hali ya
hewa sawa. Maofisa
wa Barca wanahaha kumshawishi Neymar kubaki klabuni hapo, na baada ya mchezo wa
Jumamosi usiku baba wa Neymar alikutana na Bodi ya Barcelona katika kikao
kizito kilichofanyika katika hoteli ya klabu hiyo.
...akiwa na Messi
PSG
imeshikiria msimamo wake kuhusu uhamisho huo, lakini ikijiamini kufanya
uhamisho huo mkubwa na wa kushtua. Katika
miaka ya nyuma United imejaribu kumsajili Neymar mara kadhaa bila ya mafanikio.
Post a Comment