HOUSTON, MAREKANI
DAVID DE GEA
(pichani chini) ataendelea kulinda milingoti mitatu ya Manchester United msimu ujao na atakuwa
bora kuliko siku za nyuma, Jose Mourinho ameahidi, wakati kipa huyo akijiandaa
kucheza dhidi ya Real Madrid usiku wa Jumapili.
Kipa De Gea kwa muda
mrefu amekuwa akihusishwa kutaka kurudi nyumbani kwao Hispania kujiunga miamba
hiyo ya La Liga.
Ni kucheleweshwa kwa taratibu
za utawala zilizookoa De Gea kujiunga na Madrid mwaka 2015 baada ya pande mbili
kukubaliana siku ya mwisho ya usajili.
Lakini sasa Kocha Mourinho
amedokeza United ilifungua dili la kumuuza kipa huyo katika usajili wa majira
ya joto unaoendelea, lakini Madrid haikushawishika na dili hilo.
"Naweza
kuhakikisha msimu huu hataondoka, naweza kusema hivyo," alisema Mourinho kabla
mchezo wa Jumapili dhidi ya timu hizo.
Mbali na mchezo huo, Man
United na Madrid ndani ya wiki tatu zitakutana tena mjini Santa Clara, katika kuwania
Uefa Super Cup Agosti 8.
"Aliwasilana na
klabu kwa muda mrefu, lakini hatukuwa tayari, kisha baadaye tulimkubalia, kwa
sababu kila siku ninajua hisia za wachezaji wanaotaka kuondoka, sipendi
kuwazuia kwa sababu hutapata kile unachokitaka kutoka kwao ukiwazuia.
Nina uhakika asilimia 100, atabaki nasi.
"Kwa hiyo tukairuhusu
(Real Madrid) na haikuonyesha nia, na sidhani kama (De Gea) alijisikiavizuri
kwa kitendo hicho.
"Nimemuana akiwa
na furaha kubaki hapa, anajituma na kufanya kazi kwa bidii, tofauti na siku za
nyuma. Nina uhakika kwa asilimia 100 kuwa atabaki nasi."
Kipa De Gea ameshinda
tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa miaka mitatu mfululizo kati ya mwaka 2014 na
2016.
Hata hivyo, Mourinho anaamini
kiwango cha kipa, Sergio Romero –aliyesaini mkataba wa miaka minne wiki
iliyopita- akiwa kipa aliyeipa taji la Europa League United msimu uliopita
kimemsukuma De Gea kupambana.
Romero ndiye aliyemfanya De Gea kuwa vizuri.
"Nadhani mambo
mazuri yanayotokea kwa David (Ge Gea) ni kutokana na Romero alivyocheza msimu
uliopita kwa sababu hadi wakati huo, David namba yake ilikuwa salama," aliongeza
Mourinho.
"Anafanya
mazoezi tofauti na yuko vizuri kuliko wakati mwingine, ana hali ya kushangaza
na kuvutia. Kuna nao wote katika viwango bora ni jambo zuri."
Post a Comment