BARCELONA, HISPANIA
NEYMAR amewaambia
mastaa wenzake wanaotengeneza kombinesheni hatari ya ‘MSN’ ndani ya kikosi cha
Barcelona, Lionel Mess na Luis Suarez kuwa atabaki klabuni hapo.
Taarifa kutoka
Hispania zinasema Neymar amewaambia Messi na Suarez kuwa atabaki Barcelona baada
ya mastaa hao kumweka chini kuhusu uamuzi wake wa kutaka kutimkia PSG.
Mwishoni mwa wiki habari
kubwa ilikuwa ni matajiri wa Qatari wanaoimiliki Paris Saint Germany (PSG) kuwa
tayari kulipa kiasi cha Pauni 195 milioni kinachomrushu staa huyo wa kimataifa
wa Brazil kuondoka Barcelona.
PSG ilikuwa tayari
kumlipa Neymar Pauni 25 milioni- kwa mwaka kama angemwaga wino kuwatumikia mabingwa
hao wa Ufaransa.
Rais wa Barcelona,
Josep Bartomeu alisisitiza straika huyo mwenye umri wa miaka 25-hakuwa sokoni, ingawaje
Neymar mwenyewe amebaki na shaka na maisha yake ya baadaye.
Mazungumzo kati ya
Neymar na mastaa wenzake wa Barcelona walioko katika maandalizi ya msimu mpya
Marekani, yalichukua takribani saa moja kwa mujibu wa Mwandishi wa Hispania, Toni
Frieros.
Watatu wanaounda MSN
Messi na Suarez walimshawishi
Neymar kuachana na ofa ya PSG na kuendelea na maisha yake Barcelona.
Pia, staa wa wapinzani wa jadi wa Barcelona, Cristiano Ronaldo naye alimshauri kupitia Mtandao wa WhattsAp Neiymar kubaki Barca.
Nabaki Barcelona
Ronaldo alidai PSG ni timu ndogo na bora angejiunga na Real Madrid au Manchester United kama akitaka kuondoka Barcelona.
Staa huyo alidai PSG isingeweza kumpa umaarufu mkubwa Neiymar kama ambao angeupata Man United.
Awali ilidaiwa Rais
wa Barcelona Bartomeu aliwaomba mastaa hao kuzungumza na Neymar ili kumsihi
asikubali kuchana na klabu hiyo baada ya kushindwa kufanya hivyo.
Ronaldo
Kwa sasa Barcelona imepumua
baada ya kauli hiyo inayohitimisha tetesi hizo za uhamisho. Na msemaji wa miamba hiyo ya Hispania alisitiza
kuwa Neymar hatauzwa.
“Kumuuza Neymar siyo kitu ambacho
klabu inachokifikiria,” alisema Josep Vives katika mkutano na waandishi wa
habari. “Tuna utulivu sana. Ni mmoja kati ya wachezaji muhimu tuliyenaye, hatutazingatia ofa yoyote itakayoletwa kwa ajili yake.”
Post a Comment