0


            LOS ANGELES, MAREKANI
MANCHESTER CITY imethibitisha kumnasa beki Benjamini Mendy (pichani chini) kutoka Monaco kwa ada iliyovunja rekodi ya dunia kwa mabeki ya Pauni 51.6 milioni. Beki huyo ametua Los Angeles na kusaini dili la miaka mitano baada ya klabu kukubaliana ada ya uhamisho. Mendy alijiunga na Monaco miezi12 iliyopitakwa dau la Pauni 5.5 milioni– na City imelipa karibia mara 10 ya dau hilo kuipata saini yake.

Katika usajili huu wa majira ya joto City imetumia jumla ya Pauni 213.6 milioni, baada ya Kocha wa Pep Guardiola kuwaruhusu kuondoka Pablo Zabaleta na Gael Clichy. Man City imeshawasajili Bernardo Silva, Ederson, Kyle Walker na Danilo na wanatambua watakuwa na mashindano mawili msimu huu Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa. Mendy, 23, atavaa jezi No 22 uwanjani Etihad na atakuwapo uwanjani dhidi ya Real Madrid Jumanne.Beki huyo aliema : “Bila shaka nina furaha sana kujiunga na Manchester City. Nina uhakika baada ya miaka michache tutafanikiwa.”

....akiwa uwanjani
Mendy alianza kusakata soka Ufaransa akiwa na Le Harve kabla ya kujiunga na Marseille mwaka 2013. Mkurugenzi wa soka wa City, Txiki Begiristain alisema: “Benjamin ana viwango vyote wakati tulipokuwa tukiangalia beki wa pembeni. Kwa mchezaji kijana kama yeye, ana utajiri wa afya ya kiwango cha juu na uzoefu.

... akiwa an mabosi wa Man City.
“Hana shaka kuwa mmoja kati ya mabeki bora wa pembeni, alikuwa chaguo letu la kwanza katika nafasi hiyo. Tuna furaha kuwa naye Manchester City. Nina uhakika atathibitisha kuwa ni ingizo bora katika kikosi.”

Post a Comment

 
Top