LOS
ANGELES, MAREKANI
JOSE MOURINHO ameweka
alama ya taadhari kumnasa kinda wa Bayern Munich, Renato Sanches. Kiungo
huyo Mreno alikuwa katika mipango ya bosi huyo wa Manchester United na naweza
kuruhusiwa kuondoka msimu huu kwa mkopo.
Bosi
wa Bayern, Carlo Ancelotti anataka kufanya mazungumzo na kinda huyo mwenye umri
wa miaka 19- kuhusu maisha yake ya baadaye baada ya ziara ya maandalizi ya
msimu barani Asia.
Ancho
(Ancelotti) alisema: “Pindi tukiwa na muda wa kufanya uamuzi wa pamoja kutakuwa
na uwezekano wa kumtoa kwa mkopo. Pia, uwezekano wa kubaki na kutusaidia.
“Dirisha
linafungwa Agost 31, kwa muda huu yuko nasi na anafanya mazoezi nasi.”
United
ilikuwa na mpango wa kumsajili Sanches mwaka mmoja uliopita, kabkla Bosi Louis
van Gaal kutimuliwa Old Trafford. Na
kinda huyo akawahiwa na Karl-Heinz Rummenigge na Bayern badala ya United iliyomchukua
Mourinho. Lakini
Sanches hajafanya vizuri Bayern, na baada ya Old Trafford kufanya uchunguzi wa
kina, United ina uhakika inaweza kumfanya kiungo huyo kuwa bora duniani.
Renato
Mourinho
alichanganyikiwa kwa United kuhsindwa kumnasa Sanches mwaka jana, pamoja na
kwamba wanamtumia wakala mmoja. Lakini
sasa nafasi ya kocha huyo Mreno kufanya
kazi na kinda ni kubwa sana kwa sasa kuliko wakati mwingine.
Hata
hivyo, Mourinho alikaririwa Aprili akisema: “Tunataka vijana kucheza na kufanya
vizuri.
Mourinho anahitaji vijana wanaojituma.
“Wakati huohuo, timu bora zinataka kushinda na ni vigumu kushinda ukiwa na vijana wanaojifunza. Unapaswa kwenda katika klabu zinazoendeleza vijana.
Renato anachezea benchi, Bayern
“Ni
rahisi pindi kunapokuwa hakuna presha ambapo unashinda leo, unapoteza kesho. Ni
tofauti na klabu kubwa. Kuna
kinda Mreno, Renato Sanches, aliyecheza Kombe la Euro. Lakini hapati nafasi Bayern
Munich. Mechi ya mwisho aliyocheza, wamepoteza Hoffenheim.
“Anaweza
kucheza Ligi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya? Nina wasiwasi. Unajua
kuna tofauti kati yetu sote.”
Post a Comment