LOS
ANGELES, MAREKANI
CRISTIANO
RONALDO (Pichani chini) amewataja wapinzani wake wanne kuelekea Tuzo ya Ballon d’Or mwaka 2017.
Straika huyo wa
Real Madrid mwenye umri wa miaka 32- aliwashinda Lionel Messi na Antonie
Griezmann mwaka uliopita baada ya kutwaa
taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la Ulaya akiwa na klabu yake na timu ya
taifa.
Na baada ya mwaka
mwingine wa mafanikio klabuni Real Madrid, unaomuacha Ronaldo akitwaa taji lake la pili
la Ligi ya La Liga na taji lake la tatu
la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Mreno huyo anaonekana anajipanga kutwaa kwa mara ya tano Tuoz ya Ballon d’Or –
lakini anakiri kuna upinzani.
"Bila shaka siku zote huwa ni
mpambano kati yetu. Niko sambamba na (Lionel) Messi, Neymar, (Robert)
Lewandowski na (Gonzalo) Higuain."Aina hii ya mchuano na ushindani unatia matumaini na kinachonishawishi, ni kuwa bora zaidi yao mwaka baada ya mwaka.
"Mtu bora kila siku anajaribu kushinda na watu bora, inakufanya uwe shapu. Unajua uwezi kupoteza mwelekeo kwa sababu watakupita."
Post a Comment