LOS
ANGELES, MAREKANI
MANCHESTER
UNITED mambo yake yamenoga huko Los Angeles kwenye maandalizi yao ya msimu ujao
wa Ligi Kuu England baada ya mastaa wa timu hiyo kuonekana wakiwa kwenye kambi
matata.
Kocha,
Jose Mourinho aliungana na mastaa wake wapya kwenye mazoezi hayo, huku kila
mchezaji akionekana kuwa katika ari na morali kupiga tizi la kuwaweka fiti
mapema kabla ya ligi kuanza.
Katika
mazoezi hayo, hakukuwa na mzaha na hayakuwa ya mchezo mchezo, ambapo Mourinho
aliwagawa wachezaji wake katika makundi tofauti tofauti kulingana na matakwa ya
mazoezi aliyokuwa akiwafanyisha mastaa hao.
Straika
mpya, Romelu Lukaku naye alikuwa kwenye mazoezi ya timu hiyo ambapo aliungana
na wenzake wapya kujiandaa na mambo ya msimu mpya. Staa mwingine mpya ni beki
wa kati, Victor Lindelof.
Man
United chini ya Mourinho bado wapo sokoni kusaka wachezaji wengine wakisaka
kiungo mkabaji na winga, ambapo wachezaji hao wanatajwa kuwa ni Eric Dier wa
Tottenham na Ivan Perisic wa Inter Milan.
Mastaa
karibu wote walikuwapo mazoezini huku Man United ikijiandaa na mechi yake ya
kwanza ya kupasha Julai 15 kwa kumenyana na LA Galaxy katika Uwanja wa Stubhub
Centre.
Post a Comment