LONDON,
ENGLAND
MESUT
OZIL amemtumia meseji Alexis Sanchez akimtaka abaki kwenye timu hiyo msimu huu.
Ozil
amemwambia Sanchez kwamba kama ataamua kuondoka basi jambo hilo litatibua
mipango ya Arsenal katika kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England msimu ujao.
Staa
huyo wa Chile amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake wa sasa klabuni Arsenal
huku kukiwa na taarifa kwamba Manchester City wanafukuzia saini yake.
Wiki
iliyopita, kulikuwa na ripoti zikidai Sanchez amemwambia Kocha Arsene
Wenger dhamira yake ya kutaka kwenda kuungana na Pep Guardiola, kabla ya
Mfaransa huyo kukanusha akisema hajawahi kuambiwa kitu kama hicho, wala Sanchez
kusema kama anataka kuondoka.
Wenger
hafikirii kabisa kumpiga bei fowadi wake huyo kwenye dirisha hili la usajili na
wakati Ozil akionekana kwamba atabaki hapo, anadaiwa kumshawishi mwenzake
wabaki wote ili kuipa taji la Ligi Kuu England Arsenal msimu ujao.
Ozil akiwa na Sanchez
“Nadhani
Alexis atabaki, lakini sijui nini mipango yake,” alisema Ozil.
...lakini kama ataondoka sawa tu.
“Mimi
nampa thamani kubwa kama mchezaji hasa ukizingatia amekuwa akiingia vyema
kwenye mfumo wa kiuchezaji wa Arsenal. Kwa upande wangu nataka abaki, lakini
hilo lipo juu yake mwenyewe.”
Post a Comment