LONDON,
ENGLAND
ANTONIO
CONTE hatimaye amefanikiwa kushinda vita baada ya Chelsea kukubali kuvunja
rekodi ya klabu na kulipa ada ya Pauni 68 milioni kwa Real Madrid kumnasa
Alvaro Morata.
Morata
anatarajia kuondoka katika kikosi cha Madrid kilichopo katika maandalizi ya msimu
Marekani ili kukubaliana maslahi binafsi na mabingwa hao wa Ligi Kuu England.Kukamilika kwa dili hilo la Morata kutamaliza wiki kadhaa za kuchanganyikiwa kwa Conte akimtazamia straika huyo kuwa nyenzo yake ya kutetea ubingwa msimu ujao.
Pia, usajili huo unamaaanisha Conte ameshinda vita ya Diego Costa ambaye sasa atakuwa huru kukubaliana dau kurudi katika timu yake ya zamani ya Atletico Madrid.
Makubaliano kati ya Madrid na Chelsea kumsajili Morata yamekuja saa 24 baada ya Conte kusaini mkataba ambao utaongeza msharaha wake mara mbili hadi Pauni 10 milioni kwa mwaka. Morata amepambana kuitumikia timu yake ya Real Madrid ingawaje sasa yuko tayari kuanza maisha katika soka la Kiingereza chini ya Conte msimu ujao.
Morata akiwa na mkewe, wakitua London
Staa
huyo ambaye amekulia Real Madrid kabla ya kupelekwa kukomazwa Juventus ya
Italia alionekana akiwaaga mashabiki na wachezaji wenzake wa huku akiwatakia
mafanikio.Chelsea imetua China Jumatano asubuhi kwa safari ya maandalizi ya msimu mpya baada ya kukamilisha usajili wake wa nne katika majira haya ya joto.
...akiwa na wakala wake.
Wachezaji
wengine ni beki mpya Antonio Rudiger aliyeambatana na timu hiyo Mashariki ya
Mbali sambamba na kipa Willy Caballero.Kiungo Tiemoue Bakayoko yuko nyumbani kwao akiuguza mshono wa kifundo cha mguu.
...akiitumikia jezi ya Madrid
Morata
(24), alikuwa akiongoza katika chaguo la kumrithi Costa kikosini Chelsea kwa
miezi kadhaa ingawaje timu hiyo ilishindwa dau la Pauni 75 milioni lililowekwa
na Everton kumnasa Romelu Lukaku ambaye amejiunga na Manchester United.
...akifanya mazoezi Madrid
Straika
wa Chelsea, Costa aliambiwa na Conte mwezi ulioisha kuwa hayumo kwenye mipango
yake kupitia ujumbe mfupi (SMS) na tangu wakati huo wawili hao hawajaonana uso
kwa uso.
Kwaheri, Morata akiagana na kocha wake Zidane.
Post a Comment