LISBON, URENO
STRAIKA wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ameripotiwa kuwa baba wa watoto pacha kutoka kwa mwanamke ambaye hajafahamika.
Kwa mujibu wa runinga ya Ureno, watoto hao, wa kiume na kike wanaofahamika kwa majina ya Eva na Mateo, walizaliwa Alhamisi .
'Mateo na Eva, ndio majina ya pacha wa Cristiano Ronaldo," kilidai kituo hicho cha runinga. " Watoto hao wamezaliwa na mama asiyefahamika. Ni siri ambayo Ronaldo hajaiweka hadharani."
Hata hivyo, kituo hicho hakijasema kwa uwazi watoto hao wako wapi kwa sasa na kudai hakuna picha zao hadi sasa.
Hakuna uthibitisho wowote kutoka kwa upande wa maofisa wa Ronaldo au wakala wake kuhusu habari hiyo, lakini mitandao kadhaa ya Ureno na magazeti likiwemo lile linaloongoza kwa mauzo kila siku la Correio da Manha liliandika habari hiyo Ijumaa iliyopita.
Gazeti moja la Uingereza liliwahi kuandika mwezi Machi kwamba Ronaldo alikuwa akitarajiwa kuwa baba watoto pacha wakiume.
Ilidaiwa mwanamke asiyetambulika Magharibi mwa Pwani ya Marekani ni mjamzito na alikuwa akitarajiwa kujifungua watoto hao wakati wowote.
Ronaldo anayetoka na mrembo wa Hispania Georgina Rodriguez, aliushtua ulimwengu Julai mwaka 2010 baada ya kutangaza kupitia Mitandao ya Kijamii ya Twitter na Facebook kwamba amekuwa baba.
Georgina akiwa na Ronaldo. Eti ni mjamzito?
Mtoto huyo, Cristiano Ronaldo Jr, anayejulikana kama Cristianinho, sasa ana miaka sita.
Mama wa Ronaldo, Dolores Aveiro aliweka wazi kwamba alimchukua mtoto huyo kutoka katika hospitali binafsi jijini Florida, Marekani Julai 2014 na kutua naye Ureno .
Familia ya Ronaldo imekuwa ikikataa kuzungumzia suala la mtoto huyo kuzaliwa na mama asiyefahamika, ingawaje kuna madai kwamba dada wa Ronaldo, Katia aliwahi kumwambia mtoto huyo kuwa amezaliwa na mama wawili ambao ni raia wa Mexico.
Mfanyakazi wa ndani wa Katia, Maria Manuela Rodriguez ambaye alifanya kazi mjini Moita karibu na Jiji la Lisbon kwa miezi 10 , aliliambia Gazeti la Correio da Manha mwezi Agosti 2011: " Mama wa mtoto alikuwa anataka aruduishiwe mwanaye."
Katia alijibu mapigo kwa kukanisha madai hayo: "Huo ni uongo, kwa sababu mama wa mtoto ni raia wa Mexico na hata hakumuona (mtoto) kama alikuwa wa kike au wa kiume, kwa sababu alikuwa ni mama asiyefahamika.”
Kama haitoshi Katia alidai Ronaldo aliwahi kumwambia kuwa, Cristianinho ni mtoto wa mama wawili.
Georgina akiwa na mtoto wa Ronaldo
"Aliniambia (mtoto) ana mama wawili, kwamba mayai yalitolewa kwa mwanamke mmoja na kupandikizwa kwa mwingine ambaye alibeba ujauzito na kujifungua. Na wote walikuwa raia wa Mexico.
"Mtoto alizaliwa katika hospitali binafsi na mama yake wala hakumuona, kwa sababu alikuwa amezibwa. Baada ya kujifungua hakujua chochote kuhusu mtoto huyo."
Ronaldo alichukizwa na makala ya gazeti hilo na kuchukua hatua za kisheria juu ya makala hiyo, na kudai gazeti hilo liliingilia uhuru wake binafsi.
Mahakama ya Lisbon ilitoa hukumu na kukubaliana na Ronaldo na kulipiga faini gazeti hilo, mfanyakazi huyo wa ndani na waandishi wawili walioandika makala hiyo.
Rufaa dhidi ya uamuzi huo uko katika hatua za mwisho.
Hata hivyo, Ronaldo hakuchukua hatua zozote kuhusu habari zilizomhusu mama wa mtoto wake ambazo zilikuwa zikipewa uzito mdogo Ureno, ikiwemo ile iliyodai mama huyo ni Mmarekani masikini, baameidi ambaye alilipwa Pauni10 milioni ili kutunza siri na alikabidhi mtoto huyo baada ya kukaa naye kwa usiku mmoja.
Ronaldo, Georgina na Cristiano JR
Julai 2010 Gazeti la Sunday Mirror liliripoti wawili hao walikutana katika mgawaha Los Angeles wakati Ronaldo akiwa safari kwenda Marekani na kupanga mpango huo.
Akizungumza Julai 2014, dada mkubwa wa Ronaldo, Elma alikiri : "Kuna wakati mtoto huwa anaulizia kuhusu mama yake . Mara moja tulimwambia kuwa yuko peponi, lakini kaka yangu na mama hawakupendezwa na hilo na kutukataza tusirudie tena.
"Sasa tunamwambia mama yake amesafiri. Ananyamaza kimya, anasahau kuhusu hilo na haulizi tena.”
Wakati hayo yakiendelea kuna tetesi kwamba mchumba wa sasa wa Ronaldo, Georgina Rodriguez ni mjamzito.
Mei mwaka huu, Ronaldo alisababisha watu kuzungumzia zaidi jambo hilo baada ya kuposti picha katika mtandoa wa Instragram akiwa na Georgina .
Straika huyo alionekana katika picha hiyo akiwa ameweka mkono katika tumbo la Georgina na kuandika maneno :Eti mjamzito?"
Lakini mama yake Dolores Santos amekuwa akisistiza kwamba huo ni mkono tu tumboni na haumaanishi kitu chochote.
Ronaldo sasa atakuwa baba wa watoto watatu.
"Ni upumbavu tu," alisema. "Ni mkono tu katika tumbo na kwa jinsi ninavyojua, Ronaldo hatakuwa baba kwa mara nyingine."
Baadaye, Georgina aliposti picha katika mtandao wa Instagram akiwa kwa madaktari siku chache baada ya kusambaa kwa tetesi kwamba ni mja mzito, lakini alionekana akiwa kwa Dr Rafik Dehni ambaye ni mtaalamu wa upasuaji na kutibu magonjwa ya ngozi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment