MANCHESTER, ENGLAND
ZLATAN IBRAHIMOVIC ameshaonyeshwa mlango wa kutokea Old Trafford, hivyo Manchester United inahaha kusaka saini ya No.9 na iko mbioni kukamilisha dili la straika wa Real Madrid, Alvaro Morata.
Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema Morata anasaka nafasi ya kucheza kwa muda mrefu baada ya kuanza michezo 14 tu ya ligi msimu uliopita akiwa na Real Madrid.
Inafahamika kuwa Man United itakamalimisha dili hilo ndani ya wiki ijayo na imekubali kutoa dau la Pauni 60 milioni.
Usajili wa Morata unakuja kufuatia kuruhusiwa kwa Zlatan Ibrahimovic kuondoka klabuni hapo baada ya kubainikia kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeraha ya goti.
wakati hayo yakiendelea klabu hiyo imefanya usajili wake wa kwanza katika msimu wa majira ya joto kwa kumsajili beki wa kati wa Benfica, Victor Lindelof.
Awali bosi wa United, Jose Mourinho alitaka Lindelof atue Old Trafford katika dirisha la Januari lakini usajili huo ulishindikana.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 22 raia wa Sweden ameigharimu United ada ya uhamisho Pauni 30.7 milna anatarajiwa kutua Manchester Jumatano kukamilisha vipimo vya afya, taratibu za uhamisho wa kimataifa na kukubaliana maslahi binafsi.
Morata
Usajili wa Lindelof unafanya uhamisho wa beki wa Burnley, Michael Keane kurudi United kushindikana. Kean aliyeanzia kusakata soka United alitaka kurudishwa kundini kwa dau la Pauni 35 milioni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment