0
                                               LONDON, ENGLAND
ARSENE WENGER amemwambia rafiki yake wa karibu kwamba, haoni kama Arsenal itashinda vita ya kumsainisha straika kinda wa AS Monaco, Kylian Mbappe.
Arsenal inapambana na Real Madrid, Manchester United na klabu miamba ya Ulaya katika kusaika saini ya kinda huyo mwenye miaka 18, ambaye msimu uliomalizika alikuwa moto kweli kweli.
Wenger alikuwa na imani ya kumnasa Mbappe, kwa sababu tu alikuwa shabiki wa timu hiyo tangu utotoni mwake, lakini sasa amekiri kuna ugumu wa kuinasa saini yake.
Wenger alionekana mjini Nice hivi karibuni na kuibua uvumi kuwa amekwenda kukamilisha dili la kinda huyo wa Kifaransa, lakini sasa amebadili upepo na kufukuzia wachezaji wengine.
Arsenal sasa imegeukia kwenye mpango wa kumsajili straika wa Lyon, Alexandre Lacazette baada ya kuona imefeli katika kumnasa Mbappe. PSG nayo imeingia kwenye mchakamchaka wa kumsajili staa huyo.

                                                                   Mbappe
Mbappe alifunga mabao 15 katika Ligue 1 msimu uliomalizika na alipiga asisti nane na kuweka rekodi pia ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo kufunga kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Post a Comment

 
Top