MANCHESTER, ENGLAND
IMEFICHUKA kwamba Manchester City imeshinda katika mbio za kumng’oa, Alexis Sanchez, kutoka Arsenal. Hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka Hispania.
Kuna mtu mmoja anaitwa, Gerard Romero, anayefanya kazi katika Gazeti la Sport pamoja na kituo cha redio cha huko Barcelona, Moguts pel Barca, amedai kwamba staa huyo wa kimataifa wa Chile, atakwenda kuungana na Pep Guardiola ndani ya siku chache zijazo.
Romero amekuwa akifuatilia kwa karibu usajili unaofanywa na Man City tangu Guardiola alipowasili kwenye timu hiyo na ndiye aliyefichua dili za wachezaji kama Leroy Sane, Gabriel Jesus, Nolito na John Stones kabla hata hawajatangazwa kujiunga na klabu hiyo.
Taarifa zilizotoka mapema Jumatano kutoka huko Chile zilisema mpango wa Sanchez ni kwenda kujiunga na Man City na si Bayern Munich. Inadaiwa kwamba kama Arsenal itaamua kumuuza Sanchez, basi itafanya hivyo kwa timu ya nje ya England.
Wiki iliyopita, Kocha Arsene Wenger, alisema hafikirii kupokea ofa ya kumuuza mchezaji huyo licha ya kwamba mkataba wake wa sasa umebakiza mwaka mmoja tu kufika ukingoni.
“Hawa Sanchez na Ozil watabaki kwenye timu na tunaaamini wataongeza mikataba yao,” alisema Wenger.
Sanchez
“Huwezi kuidhoofisha klabu na kuidhoofisha timu. Unachopaswa ni kuipa nguvu timu. La kinyume cha hapo kama utapata mchezaji mwingine wa kariba yake.”
Licha ya Wenger kubainisha hadharani kwamba kinara wake huyo wa mabao hauzwi, Arsenal imeripotiwa kuingia sokoni kusaka washambuliaji wapya akiwamo Riyad Mahrez, Kylian Mbappe na Alexandre Lacazette jambo linalofichua mambo kwamba Mfaransa huyo anazuga tu na Sanchez anaoondoka.
Guardiola alimsajili Sanchez wakati huo alipokuwa Barcelona wakati alipomnasa kutoka Udinese mwaka 2011 na sasa baada ya kumnasa mpishi Bernardo Silva kutoka Monaco kwa ada ya Pauni 43 milioni, anamtaka staa huyo wa Arsenal ili akafanye mambo klabuni kwake. Man City pia inamtaka beki Benjamin Mendy na imeshamchukua kipa Ederson na inawasaka pia Virgil van Dijk, Kyle Walker na Kylian Mbappe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment