0
                                NEWCASTLE, ENGLAND
MTOTO wa kiungo, Cheick Tiote, ameomboleza msiba wa baba yake kwa staili ya kipekee baada ya kuvaa jezi yake ya  timu ya Newcastle United ambayo mgongoni imeandikwa ‘R.I.P Daddy 24.’
Tiote alifariki dunia mwanzoni mwa wiki hii kwa matatizo ya moyo baada ya kuanguka akiwa mazoezini katika klabu yake ya huko China. Jezi yenye namna 24 ndiyo aliyokuwa akivaa Tiote kwa miaka saba aliyokuwa kwenye kikosi cha Newcastle.
Baada ya kifo hicho, Newcastle United iliwaalika familia ya mchezaji huyo na ndipo mtoto huyo alipopewa jezi hiyo. Tiote alianguka mazoezini Jumatatu iliyopita kabla ya kutangazwa amefariki saa nne baadaye akiwa hospitalini.

Cheick Tiote alikuwa kipenzi kwa mashabiki wa Newcastle na walikuwa na huzuni sana baada ya kupata taarifa hiyo. Tiote ameacha watoto watatu na mwingine akiwa njiani anakuja kutokana na mke wake kuripotiwa kuwa ni mjamzito.

Wachezaji mbalimbali waliandika meseji zao za pole akiwamo Dwight Gayle na Alan Shearer wakimtakia apumzike kwa amani. Mtoto aliyevaa jezi hiyo anaitwa Rafael.

Post a Comment

 
Top