PARIS, UFARANSA
ZINEDINE ZIDANE amefanya mazungumzo ya
siri na straika wa Monaco, Kylian Mbappe na kumhakikishia kuibomoa safu yake ya
ushambuliaji ili kumpa nafasi Real Madrid.
Ripoti kutoka Ufaransa zinasema Real
Madrid inataka kumfanya Mbappe kuwa na jina kubwa ‘Galactico’ na usajili wao wa
kwanza msimu huu wa majira ya joto.
Hata hivyo, nyota
huyo mwenye umri wa miaka 18 pia anatakiwa na klabu mbalimbali kubwa za barani Ulaya.
Gazeti la L’Equipe
limeripoti Zidane amemhakikishia nafasi Mfaransa mwenzake huyo na kuhakikishia kuwa atakuwa tayari kumuondoa Gareth
Bale, Karim Benzema au Cristiano Ronaldo.
Mpaka sasa haijulikani rasmi ni nani
atakayeonyeshwa njia kati yao ambao wanaunda jina la BBC ikimaanisha Bale,
Benzema na Cristiano.
Mbappe
Ronaldo tayari ameshapatwa na matatizo
katika majira haya ya joto na ameonekana kuwa tayari kuondoka Bernabeu.
Hata hivyo, hivi karibuni Rais wa Real
Madrid, Florentino Perez alitangaza hadharani kuwa mshindi huyo wa mara nne wa
Tuzo ya Ballon d’Or anatakiwa kutafakari mara mbili uamuzi wake.
Benzema anaweza kuwa mhanga wa jambo
hilo la kumpa nafasi Mbappe, ingawaje msimu uliopita ameisaidia timu hiyo kupata
ushindi mara mbili.
Los Blancos ilivunja rekodi ya dunia
mara mbili ilipowasaini Ronaldo na Bale.
Benzema
Pia, Zidane aliteta na Mbappe kuhusu
nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza msimu ujao.
Arsenal ilidhaniwa ndio klabu iliyokuwa
na nafasi kubwa ya kumnasa Mbappe kutokana na kuwa na uhakika wa nafasi
itakayompa nafasi kubwa ya kucheza.
Hata hivyo, Zidane amemwambia Mfaransa
mwenzake huyo kuwa Real Madrid itajengwa kupitia yeye msimu ujao.
Post a Comment