0


                       MANCHESTER, ENGLAND
KWELI Jose Mourinho hamkubali kabisa Cristiano Ronaldo.
Kwanza aliwaambia mabosi wake wasimsikilize kabisa staa huyo kwa madai kwamba anataka kuja Manchester United, anachofanya anatumia jina la timu kujinufaisha mwenyewe.
Pili akawaambia kama kuna hizo pesa za kumsajili Ronaldo, basi wasitumie tu katika usajili wa Neymar. Lakini, sasa baada ya kuona Neymar itakuwa ngumu kumpata, basi amewaambia mabosi wake, piga chini mipango yote ya kumsajili Ronaldo na itumike hata Pauni 100 milioni kumsajili straika wa Tottenham Hotspur, Harry Kane.
Kocha huyo Mreno ameweka wazi kwamba atapenda sana kumwona Kane ndani ya Old Trafford msimu ujao kuliko kumrudisha tena Ronaldo uwanjani hapo.
Ronaldo, 32, amekuwa akihusishwa na mpango wa kurudi katika klabu yake hiyo ya zamani baada ya hivi karibuni kuwaambia waajiri wake Real Madrid kwamba anataka kuondoka baada ya kubanwa sana na mamlaka ya kodi huko Hispania.
Baada ya kusikia habari hiyo, makamu mwenyekiti wa Man United, Ed Woodward, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya kibiashara aliona kuwa ni fursa tosha ya kuipa Man United pesa zaidi kwa kuandaa Pauni 100 milioni na zaidi ili kwenda kumsajili.

Lakini, Mourinho anasema kwamba kumsajili Ronaldo kwa Pauni 100 milioni na kisha unamtumia kwa kipindi kifupi tu kupoteza pesa hivyo, anahitaji mchezaji kijana kati ya Neymar au Kane na msimamo wake wa sasa anamtaka straika huyo Mwingereza, Kane akaongoze safu ya ushambuliaji sambamba na Alvaro Morata msimu ujao.
Mourinho ni shabiki mkubwa sana wa Kane na anaamini kwamba kiasi cha Pauni 100 milioni kitatosha kabisa kumshawishi mwenyekiti wa Tottenham, Daniel Levy kumpiga bei straika huyo.

Mourinho pia anapambana kukamilisha dili nyingienza Man United za kuwanasa Ivan Perisic, Fabinho na Nemanja Matic, huku James Rodriguez naye akiwa kwenye rada.

Post a Comment

 
Top