0


                          LISBON, URENO


CRISTIANO RONALDO anadaiwa kutaka kuondoka Hispania kwa mujibu wa habari kutoka nyumbani kwao Ureno. 
 Mshindi huyo mara nne wa Tuzo ya Ballon d’Or amekuwa na msimu mzuri Lakini katika majira haya ya joto amekumbana na wakati mgumu baada ya kudaiwa kukwepa kodi ya Pauni 13 milioni. 
 Pamoja na kwamba, Real Madrid imejaribu kumtetea nyota wake huyo, lakini Ronaldo anaonekana kutokuwa na furaha kuwapo Hispania.
Gazeti la A Bola la Ureno limeripoti kuwa staa huyo ameamua hatma ya maisha yake Hispania yamefikia mwisho na amewailisha uamuzi wake wa mwisho kwa Rais wa Real Madrid, Florentino Perez. 
Hii ni ishu ya pili ya staa huyo wa kimataifa wa Ureno katika msimu huu wa majira ya joto, baada ya kudaiwa kupata watoto pacha ambao mama yao hafahamiki.
Hata hivyo inadaiwa kuwa Real Madrid ilishamuweka sokoni staa wao huyo anayevaa jezi No 7 kwa dau la Pauni 157 milioni.
Kinachowashangaza wengi ni Ronaldo kutoonekana katika kupiga picha za jezi mpya zitakazotumiwa na Real Madrid msimu ujao. Ronaldo alitoka Manchester United na kujiunga na Real Madrid mwaka 2009 na ameshinda kila kitu akiwa na Madrid.
           Ronaldo akiwa na Kombe la Ligi ya Mabingwa.
Pamoja na kutimiza umri wa miaka 32, staa huyo bado yuko fiti katika kusakata soka na thamani yake sokoni inaweza kumfanya kuvunja rekodi ya dunia. Lakini hata hivyo, kuna klabu chache zinazoweza kumudu gharama yake.
Klabu yake ya zamani ya Manchester United pamoja na kwamba aliwahi kukwaruzana na kocha wake, Jose Mourinho alipokuwa Real Madrid.

                                      ...akiwa uwanjani.
Klabu nyingine ni Paris Saint Germain ambayo inaweza kumsajili kuziba pengo la Zlatan Ibrahimovic aliyeondoka katika dirisha la majira ya joto msimu uliopita. Chelsea na Manchester City zote zinaweza kumudu dau lake lakini tatizo Ronaldo siyo mtu anayeza kufiti katika mfumo wa Pep Guardiola wala Antonio Conte.
Sehemu nyingine anakoweza kwenda nyota huyo wa kimataifa wa Ureno ni katika Ligi Kuu ya China- na Ligi ya Marekani.

Post a Comment

 
Top