LONDON,
ENGLAND
AKUFUKUZAE
hakwambii toka unaaambiwa. Arsene Wenger si unamtaka Kylian Mbappe? Basi bana akaletewa
bei yake, alichokifanya kocha huyo, utacheka.
Akazitazama
hizo namba mara mbili, kisha akasema siyo ishu, akaachana naye, hapohapo
akachenji gia na sasa anapanga kuvamia klabuni Manchester United kumng’oa
straika Anthony Martial.
Wenger
aliambiwa na Monaco kwamba ili waketi chini kuanza mazungumzo kuhusu Mbappe
basi ni lazima iwekwe mezani Pauni 130 milioni kama kianzio cha mazungumzo
ndipo hapo kocha huyo Mfaransa alipoona miyeyusha na kufuta mpango wa kumnasa
staa huyo.
Dhamira
ya kuwa na Wafaransa kwenye fowadi yake ya Arsenal kwa msimu ujao imezidi baada
ya kugonga mwamba huko, Wenger amemua kumtolea macho Martial na anaamini kwamba
Pauni 40 milioni zitatosha kumng’oa mshambuliaji huyo kutoka Old Trafford.
Wenger
alitaka sana kumsajili Mbappe, lakini straika huyo kinda amezidiwa na mpango wa
kwenda Real Madrid jambo lililowafanya AS Monaco kumtajia bei kocha huyo na
kumwondoa kabisa kwenye kinyang’anyiro.
Wenger
Lakini,
kuhusu Martial haifahamiki kama Wenger atakubaliwa na Jose Mourinho kwenye hilo
hasa baada ya makocha hao wawili kuwa na upinzani mkali sana.
Antony Martial
Man
United ilimsajili Martial kutoka Monaco karibu misimu miwili iliyopita na
katika msimu uliopita alianzishwa kwenye mechi 18 tu katika Ligi Kuu England.
Post a Comment