MONACO,
UFARANSA
AS
Monaco inajipanga kumpoteza straika wao Kylian Mbappe. Lakini, Nike nao wapo
kwenye hatari ya kumpoteza straika huyo na kwenda kwa wapinzani wao Adidas.
Kila
kitu kina wakati wake na huu ni wakati wa Mbappe kukimbiza huko Ulaya ndani na
nje ya uwanja.
Wakati
staa huyo akiwindwa na klabu vigogo kama Real Madrid, Liverpool, Arsenal na
vigogo wengine kibao baada ya kucheza kwa kiwango kikubwa sana kwa msimu
uliopita ambapo alifunga mabao 26 akiwa na kikosi cha Monaco.
Staa
huyo akisababisha vita kali kwa klabu, anaibua vita nyingine kali kwa wapinzani
wawili watengeneza vifaa vya michezo, Adidas na Nike.
Mbappe,
18 amekuwa na mkataba wa Nike tangu alipoanza kucheza soka la kulipwa, lakini
wakati dili hilo likielekea ukingoni, Adidas sasa wanajiandaa kumpa dili tamu
zaidi.
Katika
hilo, kampuni hiyo ya Ujerumani inajiandaa kumfanya Mbappe kuwa mchezaji
anayelipwa pesa nyingi kwa mwaka, Pauni 4.4 milioni, kitu ambacho atakuwa
anampiku Mfaransa mwenzake, Paul Pogba wa Manchester United, anayelipwa Pauni
3.1 milioni kwa mwaka.
Post a Comment