LONDON, ENGLAND
KOCHA Mkuu wa Chelsea, Antonio Conte amekubali kubebeshwa lawama juu ya ugomvi wake na straika Diego Costa.
Kocha huyo Mtaliano alituma ujumbe maneno kwenye simu ya straika huyo kwamba, hayupo kwenye mipango yake ya Stamford Bridge, hivyo aondoke na jambo hilo linaweza kumgharimu Pauni 10 milioni akikatwa kwenye dirisha la usajili.
Chanzo cha karibu na Conte kilibainisha kwamba kocha huyo ataiomba radhi bodi ya timu hiyo kuwa alifanya ni makosa kwa kumtimua Costa kwa kutumia meseji tu.
Meseji hiyo iliwekwa bayana katika Gazeti la Hispania la AS na inasemakana iliandikwa hivi: “Hi Diego, natumai u mzima. Asante kwa msimu tuliokuwa pamoja. Kila la heri kwa mwaka ujao, lakini haupo kwenye mipango yangu.”
Conte kwa sasa anamfukuzia straika wa Everton, Romelu Lukaku ili aende kuziba pengo la Costa, lakini saini ya staa huyo Mbelgiji aliyewahi kucheza Stamford Bridge kabla ya kuuzwa kwenda Everton itaigharimu Chelsea pesa nyingi.
Conte akiwa na Diego Costa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment